NA WAANDISHI WETU
16th August 2013
Hayo yalibainishwa jana katika ripoti ya jengo hilo iliyowasilishwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Kutokana na mapungufu hayo, Kamati imemuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya ukaguzi ili kujua thamani ya fedha iliyotumika kama ilitumika inavyotakiwa.
Baada ya kumalizika kwa kikao cha kamati hiyo na Wizara, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mussa Azan Zungu, alisema wizara imefanya tathmini ya jengo na kuiwasilisha kwenye kamati ripoti ambayo imeainisha mapungufu yaliyopo.
“Mapungufu yaliyopo kwenye jengo hilo ni pamoja na viyoyozi kutokufanyakazi, vyoo kushindwa kuhimili matumizi kwa watu 1,000 kama ukumbi unavyopokea, miundombinu ya maji ni mibovu na viti ni vya thamani ndogo havina hadhi ya ukumbi huo,” alisema.
Zungu aliongeza kuwa kwa muda mrefu Kamati yake imekuwa ikiomba Wizara husika kuwapa mchanganuo wa gharama za ujenzi wa jengo hilo, lakini haikufanya hivyo badala yake wanawapa asilimia ya uchangiaji na kuwasilisha ripoti iliyoonyesha limejengwa chini ya kiwango.
Jengo hilo limejengwa kwa ubia kati ya serikali ya China iliyotoa mkopo usio na riba wa asilimia 46.05 na serikali ya Tanzania imetoa asilimia 54 na utaanza kulipwa rasmi kuanzia mwaka 2021 hadi 2031.
Kituo hicho kilizinduliwa Machi 25, mwaka huu, na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Xi Jinping, ikiwa ni moja ya mpango wa ‘Sera ya China Afrika’.
Ujenzi wake umegharimu Dola za Marekani milioni 29.7 (Sh. billion 47.5).
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment