Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, August 2, 2013

Maalim Seif: Viongozi saidieni Wajasiriamali

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad akiangalia kawa ambalo ni miongoni mwa bidhaa za wajasiriamali katika soko la Jumapili lililopo Chake Chake Pemba. Kawa hilo linauzwa shilingi 10,000
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad akiangalia kawa ambalo ni miongoni mwa bidhaa za wajasiriamali katika soko la Jumapili lililopo Chake Chake Pemba. Kawa hilo linauzwa shilingi 10,000
Khamis Haji, OMKR 
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif amesema Wawakilishi na Wabunge wa wananchi wanajukumu la kusaidia juhudi za wajasiriamali katika maeneo yao na kuwapa nguvu katika kuinua shughuli zao za uzalishaji na kuwapunguzia wananchi hali za umasikini.
Maalim Seif ametoa wito huo wakati alipofanya ziara ya kuwatembelea wajasiriamali wa vikundi mbali mbali wanaouza bidhaa zao tafauti katika Soko la Jumapili lililopo Chake Chake, Kusini Pemba.
Makamu wa Kwanza wa Rais alisema bado wajasiriamali wa Zanzibar wanakabiliwa na changamoto kubwa, ikiwemo taaluma ndogo ya uzalishaji na masoko, changamoto ambayo inaweza kupata ufumbuzi pale wawakilishi hao wa wananchi watakapoelekeza nguvu kubwa kuwasaidia.
Alisema katika baadhi ya majimbo, likiwemo Gando Kaskazini Pemba wajasiriamali wameweza kupata mafanikio ya kupigiwa mfano, baada ya Wawakilishi na wabunge wao kujitolea kuwapatia mafunzo kuhusiana na shughuli zao.
Maalim Seif alisema walimu na wataalamu wa shughuli hizo wapo na kinachohitajika ni viongozi hao wa wananchi pamoja na Serikali kuamua kutoa umuhimu mkubwa katika kuhakikisha wajasiriamali hao wanapata taaluma ya uzalishaji na masoko.
Hata hivyo, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar amesifu juhudi na moyo unaooneshwa na wajasiriamali wanaofanya shughuli zao katika Soko la Jumapili Pemba ambazo zimewezesha soko hilo kudumu, wakati masoko mengine kama hayo yamekufa.
 “Tulikuwa na masoko ya Jumapili kule Unguja na Barabara ya Lumumba Dar es Salaam, lakini yote yamekufa, kwa kweli juhudi zenu za kuhakikisha soko hili limedumu zinatia moyo sana”, alisema Maalim Seif.
Alisema Wizara za Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika, Biashara, Viwanda na Masoko pamoja na Ustawi wa Jamii, Maendeleo ya Wanawake na Vijana ni jukumu lao kuhakikisha mafunzo ya uzalishaji bidhaa zenye viwango vya juu vya ubora yanazidi kutolewa kwa wazalishaji hao.
Katika ziara hiyo, Maalim Seif alisema amabaini bidhaa nyingi zinazozalishwa na wajasiriamali hao ni nzuri, lakini hadi sasa hawajakuwa na mipango madhubuti ya kuzifanya vivutie na kujiuza, hasa kutokana na nyingi kati ya hizo kuwa na vifungashio visivyovutia wateja.
Alisema kwa kawaida wateja huanza kuvutiwa na biashara pale wanapoona umbo lake na nje, hivyo amezihimiza Wizara hizo kuweka mkakati wa pamoja wa mafunzo kwa wajasiriali hao, ili bidhaa zao ziweze kuvutia zaidi.
Miongoni mwa bidhaa zinazozalishwa na wajasiriamali hao ambao ni kutoka vikundi tafauti vya Pemba ni pamoja na vyakula vya lishe, bidhaa za matunda na mboga mboga, vipodozi, dawa asili, nguo na mapambo.
Katika risala yao kwa Makamu wa Kwanza wa Rais, iliyosomwa na Thureya Khamis Talib walisema miongoni mwa changamoto kubwa zinazowakabili ni uwezo mdogo wa kuagizia na kutengeneza vifungashio pamoja na eneo la kufanyia biashara.
Wakati huo huo, Makamu wa Kwanza wa Rais anaendelea na ziara yake ya kutembelea wagonjwa pamoja na kufutarisha wananchi katika Wilaya mbali mbali za Pemba.
Makamu wa Kwanza wa Rais akimfariji mzee Khamis Hamad Khamis ambaye ni mgonjwa huko Michakaini Pemba.
Makamu wa Kwanza wa Rais akimfariji mzee Khamis Hamad Khamis ambaye ni mgonjwa huko Michakaini Pemba.
Maalim Seif tayari amewatembelea na kuwafariji baadhi ya wagonjwa na wafiwa katika Wilaya za Mkoani na Chake Chake, ambapo leo ataendelea na ziara hizo katika Wilaya ya Micheweni na baadaye Wete, mkoa wa Kaskazini Pemba.
 

No comments :

Post a Comment