dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, January 26, 2015

CCM yasaka wasomi kugombea ubunge

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Stephen Wasira.
Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimewaomba wanafunzi wa elimu ya juu nchini kujitokeza kugombea nafasi za uongozi kupitia chama hicho.
Rai hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Stephen Wasira, mjini hapa katika hafla ya kuwapokea wanachama wapya 300 wa tawi la Chuo Kikuu cha Biashara na Ushirika Moshi (MUCO).
Wasira aliwaomba wanafunzi wa  MUCO, Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Stephano Moshi (SMUCCo), Chuo Kikuu Kishiriki cha Afya na Tiba (KCMC), Chuo Kikuu cha Kikatoliki -Mwenge), Chuo Kikuu Kishiriki cha Theolojia (Mwika) na Chuo cha Kimataifa cha Usimamizi na Utunzaji wa Wanyamapori (Mweka), kukibeba chama hicho kwa kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi za ubunge kwenye maeneo ambayo yanaongozwa na vyama vya upinzani.
Hata hivyo, Wasira ambaye pia ni mlezi wa CCM Mkoa wa Arusha hakuwapo katika hafla hiyo, lakini aliwakilishwa na Katibu wa Chama hicho mkoa wa Arusha, Kinam’hala Alphonce. 
Chama tawala katika siku za karibuni kimekuwa kikiwahamasisha vijana wa vyuo vikuu kujiunga nacho kama mkakati wa kukabili ushindani kutoka vyama vya upinzani ambavyo vilikuwa na ngome kubwa ya wafuasi kutoka vyuo vya elimu ya juu.
Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu, mkoani Kilimanjaro ambalo linaunda mikoa ya kichama ya CCM, wallimuomba Wasira awasilishe hoja serikalini ili utolewe mwongozo mpya kwa menejimenti za vyuo vikuu vikuu nchini kutovifunga vyuo wakati wa uchaguzi mkuu ujao, ili wanafunzi wapige kura wakiwa vyuoni walikojiandikisha.
Mwenyekiti wa Shirikisho hilo, Robert Saturine, alisema: “Tujiulize ni kwa nini wanafunzi wengi wa vyuo vikuu wanavipigia kura vyama vingine na wachache wanaipigia CCM. Kwa nini Moshi ambapo kuna vyuo vikuu sita, ndiko wapinzani wanaposhinda chaguzi? Lazima tujipange kama tunataka kuisaidia CCM…Nafikiri iko haja ya kutoa elimu ya uraia na upigaji kura na si kuvifunga vyuo.”
Katibu wa MUCO, Zacharia Katikilo, akisoma risala kwa niaba ya wanavyuo hao, alisema kutokana na mkakati waliojiwekea kuelekea uchaguzi mkuu, wamefikisha idadi ya wanachama 476 kutoka 176 waliokuwa wamesajiliwa na kwamba iwapo watapatiwa vyema elimu ya uraia, wanaweza kuwa msaada mkubwa kwa CCM.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment