dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, April 18, 2015

Dk Shein ashiriki Maziko ya Dkt Omar Makame Shauri

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(wa tatu kulia akijumuika na Viongozi na Waislamu mbali mbali katika kumswalia aliyekuwa katibu Mkuu Wizara ya Afya na Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Ukimwi Zanzibar Marehemu Dkt.Omar Makame Shauri katika Msikiti wa Kidombo Wilaya ya Kaskazini A Unguja kabla ya mazishi yake leo.
[Picha na Ikulu.]
 Baadhi ya wananchi na Waumini wa Dini ya Kiislamu wakilibeba jeneza la aliyekuwa katibu Mkuu Wizara ya Afya na Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Ukimwi Zanzibar Marehemu Dkt.Omar Makame Shauri aliyezikwa leo kijijini kwao Kidombo Wilaya ya Kaskazini A Unguja.
[Picha na Ikulu.]
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,Makamo wa kwanza wa Rais Maalim Seif Sherif na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi (katikati) wakiwa na Viongozi wengine na Wananchi katika mazishi ya aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Ukimwi Zanzibar Marehemu Dkt.Omar Makame Shauri aliyezikwa leo  kijijini kwao Kidombo Wilaya ya Kaskazini A Unguja.
[Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein(katikati)akitia udongo kufukia kaburi la aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Ukimwi Zanzibar Marehemu Dkt.Omar Makame Shauri aliyezikwa leo  kijijini kwao Kidombo Wilaya ya Kaskazini A Unguja.
[Picha na Ikulu.]
Waziri wa nchi, Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais anayehusika na mambo ya UKIMWI Mhe. Fatma Abdulhabib Fereji akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Ukimwi Zanzibar ZAC Dr. Omar Makame Shauri aliefariki wiki hii katika mazungumzo na Waandishi wa habari juu ya maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani ya mwaka 2011.

No comments :

Post a Comment