dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, April 9, 2015

WAZIRI GHASIA ALIANGAMIZA TAIFA, ATUMIA VOCHA YA SIMU MILIONI 25.8 KWA MWEZI!

  • KUNA mchwa ndani ya Serikali ya Rais Jakaya Kikwete. 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Hawa Abdulrahman Ghasia (49) pichani, ni miongoni mwa wanaotafuna fedha za umma serikalini, mithili ya mchwa. Anaripoti Mwandishi Maalum … (endelea).
Katika kipindi kisichozidi siku 52, Ghasia ametumia kiasi cha Sh. 25.8 milioni kwa matumizi yake ya simu ya mkononi, tena kupitia kampuni moja ya Airtel.
Taarifa hizi za waziri kutumia kiasi cha Sh. 25.8 milioni kwa matumizi ya simu moja ya mkononi, ndani ya muda usiofikia miezi miwili, zinafichuka katika kipindi ambacho serikali imekuwa ikitumia nguvu kukusanya michango kutoka kwa wananchi.
Michango mingi ambayo serikali imekuwa ikikusanya, ni ile ya maabara kwenye shule za kata, madawati, ununuzi wa vitabu, madaftari na ujenzi wa nyumba za walimu na madarasa.

Taarifa zinasema, katika maeneo mengi, maagizo ya serikali, yaliambatana na vitisho, huku baadhi ya walioshindwa kutoa michango hiyo wakifikishwa mahakamani na kufungwa.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya serikali na kampuni ya Aitel Tanzania Limited, waziri Ghasia ametumia mamilioni hayo ya shilingi kwa mawasiliano kati ya tarehe 1 Februari na 21 Machi mwaka huu.
“Kuna mambo ya ajabu sana ndani ya serikali hii. Taifa masikini kama hili, kuna viongozi wanaotumia kiasi cha Sh. 25 milioni kwa simu. Kwa kweli, umasikini tulionao ni wa kujitakia,” ameeleza Juma Said, mkaazi wa Kinondoni na mchambuzi wa masuala ya kisiasa na kijamii.
Nyaraka (Invoice) kutoka Aitel inamuonyesha Ghasia alipewa ankara ya malipo ya tarehe 1 Februri 2015, yenye Na. 29906000001374, ikielekeza serikali – Tamisemi – kulipa kwa kampuni hiyo, jumla ya Sh. 25,878,335.86.
Kwa mujibu wa nyaraka hizo, Ghasia amejitambulisha kuwa ni waziri wa Tamisemi. Anatumia anuani ya S.L.P 23, jijini Dar es Salaam; huku namba ya mteja – Customer Id – ikitajwa kuwa 1219937034.
Ghasia anatumia namba ya mlipa kodi (TIN) TIN: 100-961.520.
Chanzo changu kiliweza kuripoti kuwa kila mwaka serikali inatumia mabilioni ya shilingi kwa njia za anasa, ikiwamo malipo ya simu, usafiri, nguo na fenicha za ndani, badala ya fedha hizo kuwekezwa kwenye maendeleo.

Chanzo: Mwanahalisi.online

No comments :

Post a Comment