dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, May 3, 2015

Harambee yagonganisha Lowassa, Membe na Mizengo Pinda Zanzibar

Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda jana wakati wa Uzinduzi wa mfuko wa Uchaguzi wa Mkoa wa Magharibi mjini Zanzibar.

Vigogo wa CCM wanaotajwa kuonyesha nia ya kuwania kiti cha urais kupitia chama hicho, wamegongana mjini hapa katika harambee ya kuchangia chama hicho,  iliyosimamiwa na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.

Miongoni mwa vigogo waliokuwapo kwenye  harambee hiyo akiwemo mwenyeji wa shughuli Dk. Shein aliyechangia Sh. milioni 15,  ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikano wa Kimataifa, Bernard Membe na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.

Katika harambee hiyo, Pinda alichangia Sh. milioni 10, wakati marafiki wa Pinda, waliahidi Sh. milioni 203, Lowassa alichangia Sh. milioni 50 na Membe, Sh. milioni 10. Waziri Mkuu Pinda, Lowassa na Membe ni baadhi ya vigogo walioonyesha nia ya kugombea urais, katika uchaguzi mkuu ujao.

Wengine waliochangia kwenye harambee hiyo ni Kampuni ya Simon Group Sh. milioni 30 na Kampuni ya ujenzi ya Mecco, Sh. milioni 20.

Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri Mkuu Pinda alisema ari iliyooneshwa katika harambee hiyo inadhihirisha msemo wa ‘kutoa ni moyo si utajiri’.
Alisifu ari ya washiriki wa hafla hiyo na kueleza kuwa ilikuwa ya hali ya juu na yeye binafsi ametiwa moyo sana na kitendo hicho cha wana CCM katika harambee hiyo.

Aidha, akishukuru kwa michango iliyotokana na harambee hiyo iliyofanyika katika Mkoa wa Magharibi, Dk. Shein alisema, amefurahishwa na ari na moyo ulioonyeshwa na washiriki wa harambee hiyo ambao wamekiwezesha chama  kukusanya zaidi ya Sh. milioni 644.

Dk. Shein, aliwapongeza wapenzi wa CCM kwa moyo wa kujitolea na kukiwezesha chama hicho kutekeleza malengo yake.

Aliwaeleza wana CCM na wageni waliohudhuria hafla hiyo kuwa alikuwa na hakika wakati alipotoa rai kwa viongozi wa CCM Aprili 24, 2013, kufanya harambee kuchangia maendeleo ya chama hicho kuwa  zoezi hilo litafanikiwa.
Hadi sasa mikoa iliyokwishafanya harambee hizo ni Unguja ambayo ni Kaskazini, Kusini, Mjini na Mkoa wa Magharibi.

Kati ya fedha zilizokusanywa, Sh. 120.7 zilikuwa taslimu, milioni 490.8 ahadi na hundi ilikuwa Sh. milioni 33. Dk. Shein alichangia Sh. milioni 15, wakati mke wake, Mwanamwema Shein, alichangia Shilingi milioni tano.

Katika hafla hiyo, vitu mbalimbali vya asili pamoja na picha za kumbukumbu za kitaifa zilinadiwa ikiwamo picha ya kuchora ya Rais wa Zanzibar,  Dk. Shein, ambayo ilinunuliwa kwa Sh. milioni 23.

Kitu kingine kilichovutia katika mnada ni keki yenye rangi ya CCM ambayo mnada wake ulishamirishwa na mke wa Rais, Mama Mwanamwema Shein na hatimaye kununuliwa kwa Sh. milioni 12.
CHANZO: NIPASHE JUMA

No comments :

Post a Comment