dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, May 27, 2015

Lowassa: Bado nahitaji utajiri

  • Apinga viongozi kushabikia sifa ya umasikini 
  • Asema anawania urais ili Watanzania wajikwamue
WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, amesema anachukizwa na viongozi wenzake wanaoshabikia umasikini kuwa moja ya kigezo cha uongozi, akisema binafsi anatamani zaidi Mungu amwongezee utajiri.
Katika mahojiano maalumu aliyofanya wiki hii na Raia Mwema, nyumani kwake, Area C mjini Dodoma, Lowassa ambaye anatarajiwa kutangaza nia ya kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), mjini Arusha mwishoni mwa wiki hii, aliweka bayana pia kwamba anavutiwa zaidi na wanasiasa wawili, aliowataja kuwa ni Mwalimu Julius Nyerere na Kwame Nkrumah wa Ghana.
“Hapa nilipo, natamani Mungu anipe uwezo wa kifedha zaidi ya nilionao sasa kwani umasikini ni mbaya na si kitu ambacho mtu anapaswa kukiringia.
“Mimi nachukia umasikini na ndiyo maana nataka uongozi ili nami niweze kuwasaidia Watanzania waweze kujikwamua na hali hii. Nawataka Watanzania wenzangu kuondokana na dhana ya kuwachukia matajiri.

“Nasikia kuna baadhi ya viongozi wenzangu ambao wanajisifu kwa umasikini. Kwangu mimi, umasikini si sifa nzuri kwa kiongozi. Mimi si tajiri sana,” alisema Lowassa katika mahojiano hayo yaliyochapishwa katika kurasa za katikati za gazeti hili.
Lowassa ni nani?
Edward Lowassa alizaliwa Agosti 26, mwaka 1953 na aliteuliwa na hatimaye kupitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Waziri Mkuu mwishoni mwa mwaka 2005. Alibaki katika madaraka hayo kwa miaka mitatu tu, kuanzia mwaka 2005 hadi 2008, chini ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete.
Lowassa alisoma katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kutunukiwa Shahada ya Sanaa na kisha alitunukiwa Shahada ya Uzamili katika Masuala ya Maendeleo kutoka Chuo Kikuu cha Bath, nchini Uingereza.
Alisoma shule ya sekondari katika Sekondari ya Ilboru na kisha Sekondari ya Milambo mkoani Tabora, mwaka 1977.
Amewahi kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu wakati wa utawala wa Rais Ali Hassan Mwinyi, katika ngwe yake ya pili kama Rais wa Awamu ya Pili.
Aliwahi kujaribu bila mafanikio kuwania kuteuliwa kusaka urais kwa tiketi ya CCM mwaka 1995 na jina lake kuenguliwa katika hatua za awali, chini ya usimamizi wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere. Inadaiwa kwamba Nyerere ni kati ya watu waliokuwa wakiamini, wakati huo wa mchakato wa kusaka mgombea urais wa CCM, kwamba Lowassa hakuwa na sifa jambo ambalo analikanusha katika mahojiano hayo.
Mwaka 2000, wakati wa utawala wa Rais Benjamin Mkapa, Lowassa aliteuliwa kuwa Waziri wa Maji na Maendeleo ya Mifugo. Mwaka 2005 alitangaza kutoingiza jina lake katika kuwania kuteuliwa kuwa mgombea wa CCM na badala yake, alimuunga mkono Rais wa sasa, Jakaya Kikwete.
Lowassa alijiuzulu uwaziri mkuu Februari 7, mwaka 2008 baada ya kushauriwa na iliyokuwa Kamati Teule ya Bunge kupima kama anastahili kuendelea na wadhifa huo, baada ya kubainika uhusika wake wa kuingia mchakato wa utoaji zabuni kwa kampuni ya kufua umeme ya Richmond. Anasema katika mahojiano kwamba sakata hilo la Richmond ni kati ya fitina kubwa alizofanyiwa.
Amewahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC), kuanzia mwaka 1989 hadi 1990 na mwaka 1990 hadi 1993 aliteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu na Makamu wa Rais, anayeshughulikia masuala ya Mahakama na Bunge. Mwaka 1993 hadi 1995 aliteuliwa kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na mwaka 1997 hadi 200 aliteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia mazingira.



No comments :

Post a Comment