dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, July 29, 2015

WAZANZIBARI KWA MAMIA WAMSHUKURU MUNGU!

  • Wasema sala zao zimekubaliwa
  • Koti la Muungano linalowabana karibu litapanuliwa


Na Ngida wa Jamii Forums
Kaumu ya kitanzania iliyofurahi zaidi kwa Bw. Lowassa kuingia Chadema na kutegemewa kuwa mgombea wa uraisi wa Ukawa ni Wazanzibari.

Kama Lowassa atasimamishwa na Ukawa basi atapata kura zote za kutoka Pemba na zaidi ya 75% za kutoka Zanzibar, kwani wanavisiwa hivyo wanaeleza kuwa wamechoshwa na siasa ya ukiritimba ambayo CCM inaiendesha, hasa baada ya waasisi wa Muungano kufariki.

“Sasa tutapata Katiba tuitakayo na kwavile Bw. Lowassa atakula yamini kutekeleza ilaani ya Chadema na CUF, watoto wetu watasoma kwa kulipiwa na serikali mpaka vyuo vikuu na pia serikali tatu na kero nyengine za Muungano sasa zitazungumzika na sio tena taboo”. Hayo alieleza mwananchi mmoja alipohojiwa na muandishi wa mada hii.

Akiandika katika blog la kizanzibari, Mzanzibari mmoja akitumia lugha ya kitumbatu aliyaelezea matokeo ya siasa ya hivi sasa ya Bw. Lowassa kuungana na Umma katika kuleta mageuzi ya kisiasa nchini kuwa, “ngoma sasa inogile”, yaani ngoma sasa imenogea.

“Kwa kweli they have only themselves to blame. Bw. Chenge kachota bilioni 1.6 na bado yupo nje anatumbuwa, at least yule mama Profesa yeye alikubali kuwa zake zilikuwa za mboga. Wizi kama huu uliokuwa ukisimamiwa na CCM sasa utakoma. Hata kama wanasema Lowassa alikuwa fisadi lakini yeye sasa yupo rejuvenated na mbele ya Lissu, Dr Slaa, Mbowe, Maalim Seif, Pro Lipumba, etc yeye atafanya nini peke yake isipokwa kufuata ilaani za vyama vilivomuweka madarakani?

Ataifanya kazi kama punda na sisi wananchi ndio tutafaidika, kwani kisu kitakuwa shingoni mwake. Akifanya mchezo kachinjwa”, alimalizia mwanamama mmoja alipoulizwa, je, hali anaionaje sasa CCM inavyoanza kuaga kidogo kidogo?

“Masafari ya kila mwezi kuenda nje sasa yatakoma”, alielezea mwananchi mwengine, akimpiga kijembe JK ambae hatimizi mwezi yupo juu anaruka!

“Hali ya Zanzibar ndani ya Muungano sasa pia itaheshimika. Zanzibar itaonekana ni nchi kama ilivyo na sio jimbo la Tanganyika”, alimalizia mwananchi huyo.

Kama kweli ngoma inogile au vipi itategemea matokeo ya tarehe 25 October, 2015, lakini la uhakika kwa hivi sasa ni kuwa CCM ipo chali na miguu ipo juu kama mende aliyemwagiwa mafuta ya taa.



No comments :

Post a Comment