dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, August 31, 2015

Magufuli aichana ilani ya Ukawa.

Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli.
Siku moja baada ya vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kuzindua kampeni zake wakati wakimtambulisha mgombea urais wao, Edward Lowassa, kwa kishindo jijini Dar es Salaam, mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, ameiponda ilani yao.
 
Dk. Magufuli amesema CCM ndicho chama chenye ilani inayoeleweka na imetaja mambo yanayogusa Watanzania, na siyo sawa na vyama vingine ambvyo havina ilani na vimeshindwa kuweka vipaumbele vyao.
 
Akihutubia mkutano wa kampeni wilayani Ludewa, mkoa wa  Njombe na Ruvuma, Dk. Magufuli alisema:
“Hadi sasa hakuna ilani ya Ukawa, leo mnawapa nchi watu ambao ni vyama vinne hadi sasa havijaweka ilani.” 
Dk. Magufuli aliahidi kujenga kwa kiwango cha lami barabara ya Njombe hadi Ludewa, ambayo imeshafanyiwa upembuzi yakinifu na michoro kwa ajili ya ujenzi kuanza mwakani.
 
Mgombea huyo alisema serikali ya awamu ya tano itakuwa ya viwanda kila wilaya na kwamba itaboresha huduma za umeme, majisafi na salama, dawa mahospitalini, barabara za lami na wakulima kutokopwa mazao yao.Akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa jimbo la Ludewa mkoani Njombe na Madaba wa Ruvuma, alisema pia kila kijiji kitakopeshwa Sh. milioni 50 kwa ajili ya kutoa mikopo kwa vijana na wanawake zikiwa ni jitihada za kujikwamua na umaskini.
 
Alisema pia serikali ya awamu ya tano itapunguza kama siyo kumaliza kabisa kero mbalimbali katika jamii kama waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda kubughudhiwa na askari wa kikosi cha usalama barabarani na mama lishe kunyang’anywa mali zao.
 
“Serikali yangu itakuwa ya watu wanyonge, nitahakikisha huduma muhimi za jamii zinapatikana kwa wakati, mawaziri wangu watakuwa wa kuhudumia wanyonge,” alisema.
 
Alisema alipokuwa waziri alikuwa anaagizwa, lakini kwa sasa atagiza na akimwagiza waziri kupeleka maji sehemu fulani ni lazima afanye hivyo, vinginevyo atafutwa kazi haraka.
 
Kwa mujibu wa Dk. Magufuli,  kila awamu ya uongozi ina mambo yake na kufafanua kuwa  yaRais wa awamu ya kwanza, Mwalimu Julius Nyerere, ilikuwa na kazi ya kuleta Uhuru na kuwaunganisha Watanzania na leo wamekuwa kitu kimoja.
 
Alisema awamu ya pili, tatu na nne zimeliwezesha Taifa kupiga hatua kubwa kimaendeleo na serikali yake ya awamu ya tano itakuwa ni ya mchakamchaka wa maendeleo kwa kuwa mazingira mazuri yalitengenezwa na watangulizi wake.
 
Aliahidi kuwa serikali yake itafanyakazi na vyama vyote, kwa kuwa hakuna anayezaliwa na chama isipokuwa kinachoangaliwa ni maendeleo na kwamba vyama si msingi wa maendeleo.
 
Alisema kazi kubwa itakayofanywa na serikali yake ni kuufuta umaskini na uchumi kumilikiwa na wanyonge.
 
Kuhusu ubomoaji wa nyumba za wananchi kupisha miradi mbalimbali ukiwamo ujenzi wa barabara, alisema hapendi bomoabomoa na ndiyo maana barabara zimekuwa zikikwepesha, lakini pale inapozidi wanalazimika kubomoa na kuwataka Watanzania kuacha kujenga barabarani.
 
Akiwa wilayani Ludewa, Dk. Magufuli  alipokelewa na waendesha bodaboda umbali wa kilomita moja kabla ya kufika eneo la mkutano.
 
Alipofika uwanjani alipokelewa na vikundi vya ngoma sita aa aina tofauti huku wananchi wakiwa wamevalia sare za CCM na kofia huku wakiwa na bendera zenye picha za marais wa awamu ya kwanza, pili, tatu, nne na ya mgombe huyo ikiwa kubwa katikatika.
 
Kila mara wananchi hao wlisikika wakimsifia mbunge wao anayemaliza muda wake katika jimbo la Ludema, Deo Filikunjombe, wakisema kuwa ni jembe. 
 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment