dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, October 8, 2015

Pinda aonya wanaoilinganisha Rwanda na Tanzania!



Waziri mkuu, Mizengo Pinda
By Seif Kabelele
Dar es Salaam. Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) amewaonya Watanzania wanaobeza juhudi za kuleta maendeleo zilizofanywa na Serikali tangu wakati wa uhuru.
Pinda alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na wakazi wa Usevya na vijiji vya jirani kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Usevya, Wilaya ya Mlele, mkoa wa Katavi.
 “Ukubwa wa nchi ya Rwanda ni kilometa za mraba 27,000 wakati ukubwa wa Tanzania ni km za mraba 945,000 ambayo ni kubwa mara 35 zaidi ya Rwanda. Ukubwa wa Rwanda ni sawa na wilaya moja tu ya Mlele ambayo ina ukubwa wa kilometa zaidi ya 29,000. Hivi tuna wilaya ngapi hapa nchini ambazo ni kubwa kuliko Rwanda?, alihoji Pinda.
“Acheni tabia ya kulinganisha “vinchi” vidogo na Tanzania. Kazi ya kuleta maendeleo siyo ndogo. Tunamhitaji Dk Magufuli ili aweze kuleta maendeleo kwa kasi hapa nchini kwa sababu yeye ni mchapakazi na kila mmoja wetu anatambua hilo, hataki mchezo na kazi na hata wapinzani wanalitambua hilo,” alisema pinda
Pinda alisema pia anashangaa kusikia watu wakijitapa kuwa watendesha nchi kwa kasi ya ajabu na kwamba ndani ya siku 100 watamaliza shida zote na kuondoa umaskini miongoni mwa Watanzania”
“Kazi ya kuongoza nchi inataka umakini, uzoefu na watu waliobobea kwenye uongozi. Hii si kazi ya majaribio hata kidogo. Eleweni kuwa changamoto ni sehemu ya maendeleo. Tuaminini CCM na tupeni nafasi tufanye kazi kwa kumpa kura zote Dk Magufuli, wabunge wa CCM na madiwani wa CCM,” alisema.
/Mwananchi.

No comments :

Post a Comment