dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, November 18, 2015

Tanzania kuingia katika mgogoro wa Kikatiba

Image result for parliament of tanzania
Wanasheria wameonya kuwa Tanzania itaingia katika mgogoro wa kikatiba endapo Bunge la Muungano litaendelea na vikao vyake bila kuwapo uwakilishi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, wanasheria hao wakiwamo mawakili wa Mahakama Kuu, walidai kuendelea kuchagua Spika na naibu wake leo bila uwakilishi wa Zanzibar ni kuvunja Katiba.

Kukosekana kwa wawakilishi hao kunatokana na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha kufuta matokeo ya uchaguzi Oktoba 28 akisema haukuwa huru na wa haki kutokana na dosari mbalimbali lakini akasema uchaguzi wa Rais wa Jamhuri na wabunge visiwani humo ulikuwa halali.

Wanasheria hao wameegemea Ibara ya 66(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na marekebisho yake, inayoweka muundo wa Bunge unaotambua wajumbe hao.

Ibara hiyo imeainisha aina ya wajumbe watakaounda Bunge la Jamhuri kuwa ni wabunge waliochaguliwa kuwakilisha majimbo ya uchaguzi, wabunge wa kuteuliwa na wawakilishi wa BWZ.Kwa mujibu wa Ibara ndogo ya 1(c) ni takwa la kikatiba la kuwapo wabunge watano waliochaguliwa na Baraza la Wawakilishi kutoka miongoni mwa wajumbe wake, wawili wakiwa wanawake.

Wakili wa kujitegemea, Albert Msando alisema suala la wabunge watano kutoka Zanzibar siyo la akidi, bali muundo lililowekwa kwa mujibu wa Katiba.

“Katiba haikutungwa kuweka wabunge hao ili kufikisha quorum (akidi). Ni wazi kabisa wabunge hao wapo kuiwakilisha Zanzibar kama mdau wa Muungano... Hata kama akidi ipo lakini uwakilishi wa Zanzibar haupo. Hii ni dharau kwa mdau wa Muungano. Zanzibar itakuwa haijashiriki kumchagua Spika, naibu Spika wala kumpitisha waziri mkuu... Hizi ni nafasi nyeti ambazo pande zote za Muungano lazima zishiriki.”

Mwenyekiti wa Tanganyika Law Society (TLS), Tawi la Moshi, David Shilatu alisema: “Kutokuwapo kwa watu hao tunavunja Katiba. Tulitakiwa tutatue kwanza huo mgongano wa Katiba na yote haya yanatokana na kuwa na Katiba yenye mgongano mkubwa.” Wakili mwingine wa kujitegemea, Elikunda Kipoko, alisema bahati mbaya watu wanaohoji kuhusu mgogoro huo hoja zao zinapanguliwa kwa hoja nyepesi ya uwepo wa wabunge kutoka Zanzibar.

“Tuna mgogoro mkubwa wa kikatiba. Bila kuwapo kwa wawakilishi hao watano, Bunge halijakamilika. Mnakwendaje kufanya uamuzi mzito kama kuchagua Spika hao wawakilishi hawapo?” alihoji.

/Mwananchi

No comments :

Post a Comment