dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, November 28, 2015

ZANZIBAR YAIPIGIA MAGOTI MAREKANI!

NA MWINYI SADALLAH

28th November 2015
.
Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi
Siku moja tu baada ya Serikali ya Marekani kuijia juu Tanzania kwa kuitaka kumaliza haraka mgogoro wa kisiasa Zanzibar, Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi amewaomba wahisani kuyapa nafasi mazungumzo ya kutafuta muafaka wa mgogoro huo.
 
Wakati Balozi Seif akiisihi Marekani,  Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Chama cha Wananchi (Cuf), Ismail Jussa, alisema hawakubaliani na hoja ya kurudiwa uchaguzi huo wakati waangalizi wa ndani na nje wakisema ulikuwa uchaguzi huru na wa haki Mwaka huu.
 
Serikali ya Marekani imetishia kusitisha msaada wa Dola za Marekani milioni 472 sawa na Sh. 999.4 bilioni za awamu ya Pili ya fedha za Maendeleo kupitia  Shirika la Maendeleo la Milenia (MCC) la nchini humo, iwapo mgogoro wa Zanzibar hautapatiwa ufumbuzi.
 
Balozi Seif aliiambia Nipashe jana katika mahojiano maalum, viongozi wa kitaifa wamekuwa wakikutana kujadili mambo yaliyojitokeza kabla ya kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi mkuu, lengo kubwa likiwa kutafuta mufaka wa mgogoro huo.
 
Alisema mazungumzo hayo pia yanamshirikisha Katibu Mkuu wa Cuf na Makamu wa Kwanza wa Rais, Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein na viongozi wengine wa kitaifa visiwani humo.Vitisho na mashinikizo hayafai jambo la msingi mazungumzo yapewe nafasi yake katika kushughulikia suala la uchaguzi wa Zanzibar, alisema Balozi Seif.
 
Alisema mazungumzo bado yanaendelea kufanyika na wananchi watafahamishwa maazimio yake baada ya kukamilika kwa majadiliano ya pande mbili.

Hata hivyo, alisema mpaka sasa upande mmoja wa CCM ndiyo umekubali kurudiwa kwa uchaguzi mkuu kama ilivyokuwa imeamuliwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (Zec) baada ya uchaguzi wa Oktoba 25 kuharibika.
 
Alisema kuwa pamoja na nchi masikini kukabiliwa na matatizo ya kiuchumi, bado mazungumzo ndiyo njia pekee ya kutatua tatizo la uchaguzi la Zanzibar badala ya kusitisha   misaada ya kibinadamu.
 
Viongozi wengine wanaoshiriki katika mazungumzo hayo ni Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Marais wastaafu wa Zanzibar Dk. Salmin Amour Juma na Amani Abeid Karume.
 
MCC wametaka suala la Zanzibar kutafutiwa ufumbuzi kwa wakati kabla ya Bodi yake haijakutana Desemba, mwaka huu kupitia miradi mbalimbali ya Tanzania ikiwemo  Zanzibar kama sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Zanzibar imekuwa ikinufaika na fedha za MCC katika utekelezaji wa miradi ya umeme, barabara na mradi wa malaria uliokuwa ukifadhiliwa na Serikali ya Marekani na kufanikiwa kwa kiwango kikubwa kupunguza ugonjwa wa malaria kisiwani hapa.
 
Msimamo wa MCC na uchaguzi wa Zanzibar umeelezwa na Naibu makamu wa rais, wa Idara ya Operesheni Afrika, Jonathan Bloom, na Naibu Rais Makamu wa Rais Idara ya Sera na Tathimini, Thomas Kelly katika waraka wao uliokwenda kwa Mratibu wa Kanda Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi wa Tanzania nchini Marekani.
 
Aidha Marekani katika kusimamia misingi ya utawala bora, imeitaka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoa ufafanuzi juu ya sheria ya makosa ya mitandao (Cyber Crime Law) katika kipengele cha kuchapisha kanuni za utekelezaji zinazozingatia mchango wa wadau na kueleza kwa vitendo dhamira ya kulinda huru wa kujieleza.
 
Sheria hiyo imetiliwa shaka kuwa inaingilia uhuru wa kujieleza kitendo ambacho kinyume na misingi ya utawala bora baada ya kuibuka wimbi la watu kukamatwa na kufunguliwa mashitaka tangu kuanza kutumika Novemba mosi, mwaka huu.
 
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Chama cha Cuf, Jussa alisema hawakubaliani na hoja ya kurudiwa uchaguzi huo wakati waangalizi wa ndani na nje wakisema ulikuwa uchaguzi huru na wa haki.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment