dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, March 31, 2016

Fedha za MCC zingefanya haya katika michezo

Uwanja wa Taifa
By Charles Abel, Mwananchi
Dar es Salaam. Hivi karibuni Bodi ya Shirika la Changamoto za Milenia (MCC), lilitangaza kufuta ufadhili wake kwa Serikali ya Tanzania kiasi cha Dola 472.8 milioni (Sh.1 trilioni), kutokana na kutoridhishwa kwake na uamuzi wa kurudiwa kwa Uchaguzi wa Zanzibar pamoja na kutoridhishwa na Sheria ya Makosa ya Mtandao.
Fedha hizo zilipangwa kutumika katika kusaidia Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini (Rea).
Hata kama fedha hizo zisingetumika katika mradi huo, bado zingeweza kufanikisha miradi mingi ya maendeleo kama vile miundombinu ya afya, barabara, reli pamoja na elimu.
Hata hivyo gazeti hili limebaini kuwa hata sekta ya michezo ingeweza kunufaika kama fedha hizo iwapo Serikali ya Tanzania ingezipata na kuwekeza kwenye michezo.
Kwanza kiasi hicho cha fedha kingeweza kujenga viwanja 15 vyenye hadhi na ubora unaozidi Uwanja wa Taifa jijini ambao umekuwa ukitumika kwa mechi mbalimbali za kitaifa na kimataifa na riadha.
Uwanja wa Taifa ulioanza kujengwa 2003, ulimalizika na kuzinduliwa 2008 kwa gharama ya Sh57 bilioni zilizotolewa kwa pamoja kati ya Serikali ya Tanzania na China. 
Kutokana na hesabu hizo, uwanja wa kisasa wa kiwango hicho ama kuzidi, vingepatikana katika mikoa 15.
Ukiondoa viwanja vya soka, fedha hiyo pia ingeweza kugharimia ujenzi wa kiwanja kimoja cha kisasa chenye hadhi ya kimataifa kwa mchezo wa tenisi na kubakisha chenji. Mfano wa kiwanja hicho ni kile cha Arthur Ashe kilichopo nchini Marekani ambacho ndiyo kinashika nafasi ya kwanza duniani kwa ubora, kikiingiza mashabiki 23,771 huku kikigharimu Dola 254 Mil kwenye ujenzi wake.
Mchezo wa mpira wa kikapu nao ungeweza kunufaika kwa fedha hizo ambazo zinaweza kugharamia ujenzi wa viwanja viwili vya kimataifa sawa na ule wa Vivint Smart Home Arena unaotumiwa na timu ya Utah Jazz inayoshiriki Ligi ya Mpira wa Kikapu nchini Marekani (NBA). Gharama za uwanja huo ni Dola 162 mil huku ukiingiza mashabiki 19,911.
Katika kuendeleza mchezo wa ngumi, kiasi hicho cha fedha kingeweza kumuajiri kocha wa bondia, Manny Pacquiao, Freddie Roach na kumpa mkataba wa miaka 47 kufundisha ngumi nchini. Mshahara wa kocha huyo ni Dola 10 mil kwa mwaka.
Fedha hizo pia zingeweza kujenga vituo vikubwa 19 vya kisasa ambavyo vingeweza kuibua nyota wa michezo mbalimbali kama ilivyo kwa kituo cha Talisman kilichopo nchini Canada.
Gharama za ujenzi wa kituo hicho ni kiasi cha Dola 24.7 mil, huku kikitumiwa na wanariadha, wanamichezo walemavu pamoja na wanamichezo wengine.

No comments :

Post a Comment