dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, April 4, 2016

CAG: Bajeti ya serikali ipangwe kulingana na mapato ya nchi


Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Juma Assad, ameshauri upangaji wa bajeti upangwe kutokana na mapato yaliyopo.
Profesa Assad aliyasema hayo wakati akitoa mada katika semina ya wabunge wa Kamati nne za Bunge iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Alisema changamoto iliyopo sasa ni kwamba bajeti hupangwa kwa kuangalia matumizi au matakwa yaliyopo kabla ya kuangalia mapato yaliyopo.
"Kwa kuwa hatuangalii kwanza tulichonacho kabla ya kupanga bajeti, matokeo take bajeti inakuwa haitekelezeki," alisema.
Alisema changamoto nyingine za kibajeti ni pamoja na upandishaji wa bei wakati wa ununuzi wa bidhaa za umma, kushuka kwa thamani ya Shilingi na ubadilishaji wa matumzi ya fedha tofauti na bajeti ilivyoelekeza.
CAG pia mbali na kutoa elimu kwa wabunge ya jinsi ya kufuatilia utekelezaji wa Bajeti ya Serikali,  aliwataka kujiridhisha kabla ya kuchukua hatua kama kuna jambo lolote limetokea.
"Kama kuna kitu kimetokea, tujenge utaratibu wa kuhoji kwanza kitu gani kimetokea, kwa nini kimetokea, athari zake ni zipi na hatua zipi za kuchukua," alisema.
Alisema kwa kufanya hivyo, kutaepusha migogoro kutokea na kwamba kwa uzoefu hatua hizo huwa hazifuatwi.
Wakichangia mada katika semina hiyo, Mbunge wa Babati Vijijini, Jitu Sonm, alisema kama semina hizo zingekuwa zinatolewa tangu zamani, wabunge wangekuwa wanafanya kazi zao kwa umahiri.
"Vile vile semina kama hizi zingekuwa zinafanyika kuanzia ngazi za halmashauri ili na wao wajifunze jinsi ya kuandaa bajeti hali itakayofanya mfumo mzima wa kuandaa bajeti kuanzia ngazi ya chini kuwa mzuri," alisema.
Mbunge wa Viti Maalum, Felista Bura, alitaka kupatiwa ufafanuzi iwapo Ofisa Masuuli atabainika kuokoa fedha, lakini kwa kutofuata utaratibu, hatua zipi zichukuliwe.
Semina hiyo ilihusisha Kamati ya Bajeti, Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) ,Kamati ya Hesabu za Serikali  (PAC) na Kamati ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC).
CHANZO: THE GUARDIAN

No comments :

Post a Comment