Top Leaderboard Advert

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Zanzibar Diaspora

High class shops @ Fuoni

High class shops @ Fuoni

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Adsense Marquee

Wednesday, April 13, 2016

CCM sasa watakiwa kulipa kodi

By Gasper Andrew, Mwananchi 
Iramba. Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida kimewataka wafuasi wake kuwa mfano katika kulipa kodi, ushuru na michango iliyopitishwa kisheria.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM mkoani humo, Yusuf Mwandami alitoa rai hiyo juzi wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Wazazi kimkoa yaliyofanyika Kijiji cha Kinambeu, wilayani Iramba.
Mwandamizi alisema suala la kulipa kodi kwa hiari linalosimamiwa na Rais John Magufuli, iwapo litaungwa mkono na wanachama wa CCM linaweza kurahisisha kazi ya ukusanyaji mapato na kuongeza uwezo wa Serikali kutekeleza miradi ya maendeleo.
Katibu wa CCM mkoani humo, Mary Maziku alisema miaka 38 tangu kuanzishwa kwa jumuiya hiyo, imekuwa na mafanikio makubwa.
“Naipongeza jumuiya hii, sasa inakwenda vizuri ikilinganishwa na kipindi kilichopita, kidogo ifutwe. Sasa fanyeni kazi waangalieni vijana wetu wasijiingize kwenye uovu,” alisema.     

No comments :

Post a Comment