dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, April 8, 2016

Lowassa: Nchi iko katika msisimko wa muda mfupi

  • WAZIRI Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa, amesema anatiwa shaka na mustakabali wa taifa kutokana na utaratibu wa Rais John Magufuli katika kuongoza nchi.


Kauli hiyo wakati akizungumza na wanazuoni wa ndani na nje ya nchi wakiongozwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM), Prof. Rwekaza Mkandala, walipomtembelea aliitoa jana nyumbani kwake Masaki, jijini Dar es Salaam.

Lowassa ambaye mwaka jana aligombea urais kwa tiketi ya Chadema akiungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vya CUF, NCCR-Mageuzi na NLD na kubwagwa na Rais Maguli aliyekuwa akigombea kupitia CCM, alisema hali ya siasa nchini kwa sasa ni ya hamasa, lakini isiyo na msingi endelevu.

"Hali ya siasa hivi sasa ni ya hamasa kutokana na serikali mpya na 'staili' mpya, kwa kipindi kifupi atakuwa maarufu (Magufuli), lakini hakuna mafanikio ya kiuchumi mbele ya safari," alisema.Akitolea mfano, Lowassa alisema Rais Magufuli amekuwa akichukua maamuzi ya kugawa fedha kwa shughuli mbalimbali wakati chombo cha kufanya hivyo kipo ambacho ni Bunge.

"Kugawa pesa siyo kazi ya Rais, kuna taasisi ambayo ni Bunge yenye mamlaka ya kuidhinisha bajeti," alisema.

Baada ya kufuta kwa shamrashamra za Sherehe za Uhuru mwaka jana, Rais Magufuli alitoa agizo kuwa, Sh. bilioni nne, zilizokuwa zitumike katika shughuli hiyo, zielekezwa kwenye utanuzi wa barabara ya kutoka Mwenge mpaka Morocco jijini Dar es Salaam kazi ambayo ipo katika hatua za mwisho kwa sasa.

Pia, hivi karibuni akiwa mapumzikoni nyumbani kwake Chato, mkoani Geita, Rais Magufuli alitangaza kufuta sherehe za Muungano zinazotarajiwa kufanyika Aprili 26, mwaka huu, hatua aliyosema itaokoa Sh. bilioni mbili ambazo ameagiza zitumike kujenga barabara ya kuelekea Uwanja wa Ndege wa Mwanza.

Mbali na suala hilo, Lowassa alisema anasononeshwa na hali ngumu ya maisha pamoja na idadi kubwa ya watu kuachishwa kazi.

"Nasononeshwa ninapoona watu wanaachishwa kazi kwenye mashirika mbalimbali kwa sababu ya hali ngumu ya uendeshaji mashirika hayo," alisema na kuongeza:

"Bandarini sasa hivi nasikia uingizaji mizigo umeshuka kwa asilimia 50, kampuni nyingi za mizigo zimefunga shughuli zake na pale kulikuwa na vijana wetu wengi wanaajira, sasa hivi wako mitaani, hali inatisha, maisha ya mwananchi yanazidi kuwa magumu," alisema.

Kadhalika, alisema kitendo cha nchi wahisani wakiongozwa na Marekani kuzuia baadhi ya misaada yao ni pigo kwa mustakabali wa uchumi wa nchi.

"Halafu tunasema tunataka nchi ya viwanda, hela tutatoa wapi kama si hawa donors (wafadhili) wa ndani na nje kusaidia katika hilo," alihoji na kuongeza:

"Hawa donors siyo watu wa kuwabeza...they will pull us back (wataturudisha nyuma), Jakaya (Rais Mstaafu Jakaya Kikwete) kwa kiasi kidogo alijitahidi kuvutia wawekezaji, japo kulikuwa na uzembe na ufisadi katika kuwasimamia, hapa kinachotakiwa ni kufanya mabadiliko katika mfumo na kuufanya kuwa endelevu.”

"Siyo kweli kwamba kila mtu katika serikali ya Jakaya alikuwa mla rushwa, lakini ni kweli kwamba mfumo ule ulikuwa mbovu na wakifisadi."

Lowassa, ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, aliwaambia wanazuoni hao kuwa upinzani ulishinda katika uchaguzi mkuu uliopita, lakini vyombo vya dola vilipora ushindi wao.

"Uchaguzi ule tulishinda na kila mtu anajua hivyo, hata Magufuli analijua hilo, lakini walitumia vyombo vya dola kupora ushindi wetu...zilinunuliwa pingu nyingi sana kuwafunga Watanzania walioamua kuleta mabadiliko," alisema Lowassa ambaye kuhahamia kwake Chadema kulisaidia kuipa nguvu Ukawa na kuweza kuongeza kiasi kikubwa cha wabunge bungeni.

Akizungumzia mikakati yao (upinzani), Lowassa aliwaambia wanazuoni hao kuwa, wamejipanga kuhakikisha hawaporwi tena ushindi wao chaguzi zijazo na kuongeza kuwa joto la kutaka mabadiliko bado ni kubwa sana kwa kile alichosema Watanzania wameichoka CCM.

/Nipashe.

No comments :

Post a Comment