dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, April 13, 2016

Magufuli ‘amevimaliza’ vyama vya upinzani au vimepumzika?


Baada ya makala yangu ya wiki iliyopita katika gazeti hili toleo namba 5731 iliyokuwa na kichwa cha habari, ‘Kwa nini Rais wetu huji na sera hizi?’ msomaji wangu mmoja alinipigia simu na kutushangaa eti kwa nini sisi waandishi wa habari hatuandiki kuwaambia wapinzani waunge mkono kazi anazozifanya Rais John Magufuli.

Kwa mujibu wa msomaji wangu huyo, anaamini kabisa sasa hivi vyama vya upinzani ‘havina chao’ kwani mambo yote waliyokuwa wakiyapigia kelele huko nyuma ndiyo ambayo Rais Magufuli na Serikali yake wanayafanya.

Msomaji wangu huyo aliendelea kuniambia kuwa: “hebu mwandishi jiulize, tangu Magufuli awe Rais, wewe wapinzani unawasikia sasa hivi, wana jambo jipya zuri? Ni kama wamekwisha, waambieni wamuunge tu mkono Dk Magufuli.”Kama una haraka ya kutoa uamuzi unaweza ukamuona msomaji wangu ni mtu anayefikiri kwa niaba ya chama fulani, hawapendi wapinzani waliopo nchini na wala matamshi yake hayana hoja yoyote.

Hata hivyo, ukimtafakari kwa umakini utagundua msomaji wangu huyu alikuwa na hoja za msingi za kusema hivyo kuwa wapinzani sasa waongee lugha moja na Rais Magufuli pamoja na Serikaili yake.

Miongoni mwa hoja hizo ambazo mimi naweza kuzisema ni pamoja na mwenendo wa sasa wa baadhi ya vyama vya upinzani na matamshi yanayotolewa dhidi ya viongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano.

Pia, baadhi ya vyama hivyo wakati huu ‘vimefunikwa’ na kushindwa kuja hata na mipango mbadala wa kulisaidia taifa.

Badala yake, vyama hivi vya upinzani kwa sasa vimeendeleza ule mtindo wa kuishi kwa matukio wa kusubiri kiongozi mmoja wapo serikalini ateleze au atoe kauli yenye utata ndiyo viongozi wake wanajitokeza na kutoa kauli.

Jambo baya zaidi linalofanywa na vyama hivyo siku hizi ni kukosoa hata pasipo stahili kiasi kwamba wanawatia shaka wananchi na kuviona kama ni vyama visivyo na nia njema na Taifa.

Mathalan, ile kauli ya kiongozi mmoja mkubwa wa chama kimoja cha upinzani nchini iliyonukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari na kutafsiriwa ilikusudiwa kuzuia mbio za Rais Magufuli za kutumbua majipu.

Haya mwingine juzi tu kutoka huko huko vyama vya upinzani amenukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari akisema kuwa Rais anapenda umaarufu.

Sawa ni kweli Rais wetu wa sasa anaonekana kwenye vyombo vya habari, hivi hilo ndiyo ameliona jambo kubwa mno la kukosoa na lenye tija kwa Taifa.

Hivi mpaka hapa kwa nini msomaji wangu huyo na wengineo, wasithubutu kusema kuwa wapinzani hawana jipya kwa sasa.

Maana badala ya kuwaona wakitoa sera, mikakati makini ya kuliendeleza Taifa letu bila kujali hata kama watawala watawapuuza, bali wao wamebaki kukosoa na kulalama tu.

Siyo kazi ya wapinzani kumtetea Serikali
Binafsi sikubaliani na msomaji wangu huyo na watu wengine wanaotaka wapinzani wajisalimishe moja kwa moja mikononi mwa Rais Magufuli, kisa eti kuwa hawana jipya kama anavyodai.

Serikali ya Rais Magufuli siyo timilifu moja kwa moja, kwani inaongozwa na binadamu walioumbwa na Mwenyezi Mungu na huyo muumbaji alishatuambia ametuumba tukiwa dhaifu.

Ndiyo maana hata wale dada zetu wanaoimba taarabu wakatuimbia nyimbo yenye mashairi kuwa hakuna aliyetimia si mwingine bali Rahman. Neno Rahman hapa linaamanisha Mwenyezi Mungu.

Kwa msingi huo, ina maanisha hata Serikali ya Rais Magufuli itakuwa na kasoro na udhaifu kidogo jambo lipo wazi na tayari baadhi ya kasoro zimeanza kujitokeza.

Kwa mfano sasa hivi, licha ya kwamba Rais Magufuli na Serikali yake kuorodhesha ahadi lukuki za kuifikisha nchi katika uchumi wa kati na kulifanya Taifa kufikia uwezo wa kutoa hisani kwa nchi nyingine.

Ila ukitafakari kwa makini unaona kabisa bado kuna nakisi ya dira, sera na mipango ya dhati ya kufikia huko kwenye nchi ya ahadi.

Nikitolea mfano wa sera hizo, hebu tuiangalie nchi ya Malaysia wakati wakiwa na ndoto kama zetu za leo za kulifanya Taifa lao liwe na maendeleo, wao mwanzoni kabisa moja ya sera waliyokuja nayo ni ile isemayo ‘look at East’ kwa tafsri yangu ‘Tujifunze kutoka Mashariki’.

Maana ya Mashariki hapa walimaanisha nchi ya Japan, ndani ya sera hii kila Mmalaysia alipaswa kujifunza kwa hali na mali mambo waliyoyafanya ndugu zao Wajapani mpaka wakaendelea.

Wakati Serikali ya Rais Magufuli takribani miezi sita (6) sasa ikiwa ‘taabani’ katika eneo la kubuni sera na mikakati shirikishi, navyo vyama vya upinzani vimefeli huko.

Sitaki kuamini kuwa vyama hivi vinayo mikakati hiyo ila vinaificha ili kumuacha Rais Magufuli na Serikali yake watafute mipango yao wenyewe na kama wanafanya hivyo, basi watakuwa na roho mbaya na hawana nia njema na Taifa letu.

Ila kama nao hawana halafu kipindi chote hiki wao kazi yao ni kukosoa na kulalamika tu, basi sidhani kama vitakuwa vimepumzika bali vimepoteana ndani ya uwanja wa Rais Magufuli kwani vilipaswa kutuonyesha sasa hivi.

No comments :

Post a Comment