Top Leaderboard Advert

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Zanzibar Diaspora

High class shops @ Fuoni

High class shops @ Fuoni

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Adsense Marquee

Sunday, April 10, 2016

Makamu wa Rais aimwagia sifa China

Makamu wa Rais wa , Samia Suluhu Hassan, akizindua mradi wa ujenzi wa nyumba za Palm Village kwenye Ufukwe wa Msasani Dar es Salaam jana. Kushoto ni Waziri wa Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage, wa pili kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene na watu kushoto ni Mwenyekiti wa Kampuni Uwekezaji ya Group 6 Jonson Huang. Picha na Said Khamis
By Kelvin Matandiko,Mwananchi 
Dar es Salaam. Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan ameipongeza Serikali ya China kwa kudumisha urafiki wake na Tanzania na kufanikisha kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini.
Samia alisema hayo jana wakati akizindua mradi wa ujenzi wa jengo kubwa la kibiashara la Palm Village, linalojengwa Msasani kupitia Kampuni ya Kichina ya Group Six International (GSI).
Alisema uhusiano huo wa miaka mingi kupitia uwekezaji wa huduma mbalimbali za Teknolojia ya Habari na Maendeleo (Tehama), biashara na ujenzi wa majengo makubwa ukiendelea kudumishwa, utaongeza ajira kwa Watanzania na kukuza pato la ndani.
Katika uzinduzi huo, Samia alikuwa ameongozana na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Juliet Kairuki.
“Akufaaye kwa dhiki ndiyo rafiki na rafiki wa kweli, urafiki wa China na Tanzania umekuwa usiokuwa na masharti na vigingi, kupitia mradi huu nimesikia zaidi ya Watanzania 2,000 wataajiriwa hapa na wataalamu 100 wakitoka China, ila kabla ya kuondoka wakifanya kazi waturithishe ujuzi wao,” alisema.
Waziri Mwijage alisema Watanzania wanatakiwa kutumia TIC kwani kipo kwa ajili yao na siyo wawekezaji wa kigeni pekee.
Aliomba kampuni ya GSI na nyingine za ujenzi kuwekeza nguvu zao pia katika mikoa mingine ikiwamo Kigoma na Tabora badala ya kubaki Dar es Salaam.
Alipoulizwa mtazamo wake kuhusu wahisani kujitoa na ndoto ya uchumi wa viwanda, Mwijage alitumia mfano kujibu akisema: “Tuna msemo unaosema mtu anayekusindikiza halafu hawezi kukufikisha nyumbani ni afadhali aache tu ili ujue uko peke yako.”
Mkurugenzi Mtendaji wa GSI, Janson Huang alisema katika kipindi cha miaka kumi ya uwekezaji wake Tanzania, imesaidia kutoa ajira 15,000 na kuanzisha zaidi ya fursa 1,000 kupitia miradi ya ujenzi.

No comments :

Post a Comment