dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, April 11, 2016

Mawaziri wa Shein waja na mikakati mizito

Rais wa Zanzibar, Dk, Ali Mohammed Shein, jana aliwaapisha mawaziri 15 na naibu mawaziri saba wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Mawaziri hao waliteuliwa juzi, ikiwa sehemu ya ukamilioshaji wa kuundwa kwa serikali, baada ya uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi 20, mwaka huu.
Hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya Ikulu mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali na mawaziri wastaafu wa serikali iliyopita.
Wakizungumza na Nipashe baada ya kula viapo, mawaziri hao walisema watahakikisha wanawatumikia wananchi kutokana na nafasi zao ambazo wameteuliwa na rais.
Waziri wa Fedha, Uchumi na Mipango, Dk. Khalid Said Mohammed, alisema wananchi watarajie mambo makubwa ya kimaendeleo ataitumia kikamilifu nafasi hiyo kwa maslahi ya taifa.
Kuhusu changamoto ya Tanzania kutishiwa misaada na wahisani, alisema amejipanga kuhakikisha serikali inapunguza utegemezi kutoka kwa wahisani.
Alisema ili Zanzibar iweze kujiendesha bila ya kutegemea misaada kutoka kwa wahisani ni lazima kuongeza fedha kutoka katika vyanzo vya ndani na hilo atahakikisha analisimamia.
“Tutahakikisha tunaimarisha mapato kwa kupanua wigo wa upatikanaji wa mapato lakini vyanzo vilivyopo kuhakikisha tunakusanya mapato kikamilifu” alisema Dk. Khalid.
Waziri Kilimo, Maliasili, Uvuvi na Mifugo, Hamad Rashid Mohammed, alisema atahakikisha kila mwezi anapeleka ripoti ya utendaji kazi wa wizara yake kwa Rais kupitia Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais.
Alisema lazima apambane na watendaji wababaishaji ambao wako serikalini na kuhakikisha watendaji wote wanafanya kazi kwa mujibu wa majukumu yao ya kazi. Kama uwajibikaji utakuwapo hali itabadilika sana.
Hata wale wafanyakazi wavivu watakuwa hawana nafasi tena,” alisema Hamad. Said Soud, Waziri Asiekuwa na Wizara Maalum, alisema yuko tayari kufichua maovu ambayo yamejificha kwa nia ya kuisaidia Zanzibar kufikia maendeleo.
Alisema atashughulikia kilimo ambacho kitasaidia kuleta maendeleo, hasa kutumia kilimo cha biashara kama viungo ili kupata fedha za kigeni.
Waziri huyo ambaye pia aligombea urais wa Zanzibar kupitia chama cha AFP, alisema lazima serikali kuweka kipao mbele cha elimu haswa ya kumkomboa mzanzibari ambayo itaweza kumpatia maendeleo.
Majina ya mawaziri ambao wameteuliwa na Rais na jana kuapishwa ni Issa Haji Ussi ( Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi) ambaye katika serikali iliyopita alikuwa Naibu Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano, Balozi Ali Abeid Karume (Ujenzi, Mawasiliano, Uchukuzi na Usafiri) na Haruna Ali Suleiman (Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora).
Wengine ni Haji Omar Kheir (Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalumu za SMZ), Mohammed Aboud Mohammed (Ofisi ya Makamu wa Pili ya Rais) na Mahmoud Thabit Kombo (Afya).
Mawaziri wengine ni ni Khalid Salim Mohammed (Fedha na Mipango), Riziki Pembe Juma (Elimu na Mafunzo ya Amali), Balozi Amina Salum Ali (Biashara, Viwanda na Masoko), Rashid Ali Juma (Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo) na Moudline Castico (Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto). Pia wamo Salama Aboud Taib (Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira), Hamad Rashid Mohammed (Kilimo, Maliasili, Uvuvi na Mifugo) na Said Soud Said na Juma Ali Khatib ni Mawaziri wasio na wizara maalum.

/Nipashe

No comments :

Post a Comment