Top Leaderboard Advert

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Zanzibar Diaspora

High class shops @ Fuoni

High class shops @ Fuoni

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Adsense Marquee

Sunday, April 3, 2016

Mgeni Naibu Spika Zanzibar!

Image result for baraza la wawakilishi zanzibar

Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW), wamemchagua Mgeni Hassan Juma kuwa Naibu Spika katika uchaguzi uliyofanyika jana.

Mgeni alitagazwa mshindi katika uchaguzi huo na Spika wa Baraza la Wawakilishi, Zuberi Ali Maulidi baada ya kupata Kura 73 kati ya 74; akiwa mgombea pekee katika uchaguzi huo.
 
Katika uchaguzi huo, pia wajumbe wa BLW walichagua wenyeviti wa Baraza la Wawakilishi, Riziki Pembe Juma na Sheha Hamad Mattar baada ya kupata kura 73 kila mmoja kati ya kura 74 katika uchaguzi huo.
 
Kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1995 mfumo wa vyama vingi ulipoanza BLW nafasi za uongozi zilihusisha wagombea pekee baada ya Chama cha wananchi (CUF) kususia uchaguzi wa marudio na vyama vingine kushindwa kupata kiti hata kimoja katika uchaguzi huo.“Naahidi nitafanya kazi kwa ushirikiano na wajumbe wote bila ya kubagua mtu na nitafanyakazi na wafanyakzi wote wa Baraza hili,” alisema Naibu Spika Mgeni.
 
Katika hatua nyingine, aliyekuwa Spika Pandu Ameir Kificho amewasilisha waraka wa kuwaaga wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na kuwatakia kazi njema baada ya kuanguka katika hatua za awali za uchaguzi ndani ya chama.
 
Kificho katika uchaguzi wa chama wa kuwania nafasi hiyo aliagushwa na Maulidi baada ya kupata kura 11 kati ya ya 55.
 
Katika waraka wake, Kificho aliwashukuru viongozi wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM na Kamati Kuu kwa kufanikisha mchakato wa kuwapata wagombea wa nafasi ya Spika Zanzibar.
 
Alimpogeza Spika Maulidi baada ya wajumbe kuonyesha imani naye na kumpa ushindi wa kishindo na alimwombea kwa Mungu katika utekelezaji wa majukumu yake.
 
Aidha, Kificho aliwapongeza Wawakilishi na watendaji wote wa Baraza la Wawakilishi walivyompa ushirikiano katika vipindi vyote vya uongozi wake.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment