dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, April 14, 2016

Mwakilishi WHO atembelea Wizara ya Afya Zanzibar kupata tarifa za Kipindupindu

 Waziri wa Afya Mhe, Mahmoud Thabit Kombo kulia akisalimiana na Muakilishi wa Shirika la Afya Duniani WHO alioko Zanizbar Dk, Ghirmay Andemichael mara baada ya kuwasili Ofisini kwake Mnazi mmoja Mjini Zanzibar, kupata taarifa ya  maradhi ya kipindupindu yalioanza mwezi Septemba mwaka jana hapa  Zanzibar.
 Waziri wa Afya Mhe, Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na muakilishi wa Shirika la Afya Duniani WHO nchini Tanzania Dk, Rufaro Chatora kushoto yake pamoja na ujumbe aliofuatana nao Ofisini kwake Mnazi mmoja Mjini Zanzibar. Muakilishi huyo alifika kuangalia hali ya maradhi ya kipindupindu  Zanzibar.
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya Mohd Saleh Jidawi katikati akizungumza na muakilishi wa Shirika la Afya Duniani WHO Tanzania Dk, Rufaro Chatora kushoto yake pamoja na ujumbe aliofatana nao na Wakuu wa Sekata mbalimbali katika Wizara hio kuhusiana na maradhi ya Kipindupindu  Zanzibar.
Muakilishi wa Shirika la Afya Duniani WHO Dk, Rufaro Chatora katikati akizungumza na Wakuu wa sekta mbalimbali katika Wizara ya Afya Zanzibar kuhusiana na Maradhi ya Kipindupindu  Zanzibar. Kushoto yake ni Muakilishi wa WHO aliopo Zanzibar Dk, Ghirmay Andemichael na kulia yake ni Katibu Mkuu wizara ya Afya Zanzibar Mohd Saleh Jidawi.
Mkurugenzi  Kinga na Elimu ya Afya Mohd Dahoma akitoa ufafanuzi wa maswala yalioulizwa na Waandishi wa Habari kuhusiana na Maradhi ya kipindupindu  Zanzibar.

PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.
NA RAMADHANI ALI/MAELEZO ZANZIBAR          
Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Tanzaia Dkt. Rufaro Chatora amezishauri taasisi za Serikali, taasisi za kiraia na watu binafsi kila mmoja kutekeleza wajibu wake katika kukabiliana na maradhi ya kipindupindu nchini.


Amesema maradhi ya kipindupindu yanapotokea katika nchi moja yanagusa nchi nyingi duniani kutokana na watu kusafiri kutoka nchi moja kwenda nyengine katika harakati zao za maisha.


Dkt. Chatora ameeleza hayo alipokuwa akizungumza katika mkutano na watendaji wakuu wa Wizara ya Afya na waandishi wa Habari katika ziara yake ya kuangalia hali ya maradhi ya kipindupindu Zanzibar tokea yalipoanza mwezi Septemba mwaka jana hadi hivi sasa ambapo watu 2703 wamepata ugonjwa huo.


Amesema maradhi ya kipindupindu ni rahisi kutibika iwapo kila mtu atatimiza wajibu wake na kufuata ushauri wa wataalamu wa afya ikiwa ni pamoja na kuacha kutumia maji yasiyo salama ambayo ni moja ya chanzo kikubwa cha kupata maradhi hayo.



Mwakilishi huyo wa WHO amesema Shirika hilo kwa kushirikiana na mashirika mengine ya Kimataifa litaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kukabiliana na maradhi hayo ili kuhakikisha yanamalizika.


Akieleza hali ya kipindupindu ilivyo hivi sasa Zanzibar katika mkutano huo uliofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja, Mkurugenzi Kinga na ELimu ya Afya Dkt. Mohd Dahoma amesema hali bado sio nzuri na wanaendelea kupokea wagonjwa wengi katika kambi ya Chumbuni.


“Tunapokea wagonjwa kati ya 10 hadi 15 kwa siku katika kambi ya Chumbuni, kwa bahati mbaya jana tulipokea wagonjwa 20 na kambi moja mpya imefunguliwa katika kisiwa cha Tumbatu,’’ alisema Dkt. Dahoma.


Amesema jumla ya Kambi 17 za wagonjwa wa kipindupindu zimefunguliwa katika maeneo mbali mbali ya Unguja na Pemba na kumi kati yao zimefungwa baada ya kukosa mgonjwa wa maradhi hayo.


Ameongeza kuwa kati ya wagonjwa 2703 waliogunduliwa na maradhi hayo 34 wamefariki ikiwa ni sawa na asilimia 1.3 na vijana wenye umri kuanzia miaka 17 ndio walioathirika zaidi.


Dkt. Dahoma amesema kisiwa cha Unguja kimekuwa na wagonjwa wengi zaidi wa kipindupindu asilimia 52.3 na Pemba ni asilimia 47.3 huku Mkoa Mjini Magharibi ukiongoza ukifuatiwa na Mkoa Kaskazini Pemba.


Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya amewashauri wananchi kuwawahisha mapema vituo vya afya watu wanaobainika na dalili za maradhi ya kipindupindu kwa vile imeonekana wagonjwa wengi wanapopelekwa vituoni afya zao zinakuwa mbaya na matibabu yanakuwa magumu
. 

No comments :

Post a Comment