dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, April 8, 2016

Nape akiri udhaifu Sheria ya Magazeti

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, 
Nape Nnauye
By Anthony Kayanda, Mwananchi 
Kigoma. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amekiri kwamba Sheria ya Magazeti ya Mwaka 1976, aliyoitumia kulifuta Gazeti la Mawio ni mbaya inahitaji kufanyiwa marekebisho.
Akizungumza na wadau wa sekta ya wizara yake mjini Kigoma ,Nape amesema sheria hiyo iliyokuwa ikilalamikiwa na wadau wa habari kwa miaka mingi, sasa muswada wake utapelekwa bungeni ili ujadiliwe na kufanyiwa marekebisho.
Muswada huo utakaojulikana kama Muswada wa Huduma za Vyombo vya Habari, utakuwa chini ya wizara hiyo huku Muswada wa Haki ya Kupata Habari, utawasilishwa na Wizara ya Katiba na Sheria.
Ili kuondoa manung’uniko kwa waandishi na habari, wizara hiyo itaunda Bodi ya Kusimamia Maadili, Miiko na Uendeshaji wa Vyombo na kusimamia mwenendo mzima wa waandishi kama ilivyo kwa bodi za makandarasi au madaktari.
“Kama ni adhabu zitatolewa na nyie wenyewe kupitia bodi yenu, bila shaka itasaidia kupunguza makanjanja,” amesema Waziri Nape.
Amesema muswada huo umezingatia maoni ya wadau kwa asilimia 99 ya mapendekezo yao, hivyo ni unaakisi kile kilichokusudiwa na waandishi wa habari na wadau wa sekta hiyo nchini.
Pia, amezitaka halmashauri za wilaya na manispaa kuanzisha vituo vya utangazaji, ili watoe taarifa nyingi za maendeleo kwa watu na kuhamasisha ukusanyaji mapato ya halmashauri.
Waziri Nape ameagiza uongozi wa Mkoa wa Kigoma kuajiri maofisa habari kila halmashauri, wahakikishe wanashiriki vikao vyote vya uamuzi hata kama siyo wajumbe lakini waingie kama waalikwa.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali mstaafu, Emmanuel Maganga amesema mkoa una maofisa habari wanne ilhali mahitaji ni tisa, jambo linalokwamisha utoaji taarifa kwa wananchi.
Jenerali Maganga ameomba wizara kuagiza vituo vya redio na runinga kuandaa vipindi vya kuelimisha jamii, badala ya burudani hivyo kujikuta wananchi wakikosa fursa nzuri ya kujifunza njia bora za kujikwamua na umaskini.
Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) Kanda ya Kati, Eswatie Masinga amesema mamlaka imejipanga kutoa adhabu kwa vituo vya utangazaji vinavyotumia maudhui yasiyozingatia maadili, hivyo kwenda kinyume na utamaduni wa Mtanzania.
Masinga amesema Kigoma umepangiwa nafasi nane za kuanzisha vituo vya utangazaji, kila wilaya imepangiwa nafasi mbili, akitaja wilaya zitakazonufaika na mpango huo kuwa ni Kigoma, Kasulu, Uvinza na Buhigwe.   

No comments :

Post a Comment