dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, April 12, 2016

Polisi wanne wafukuzwa, washtakiwa kwa rushwa

By Robert Kakwesi, Mwananchi 
Urambo. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Mkoa wa Tabora leo imewapandisha mahakamani polisi watatu kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa ya Sh3 milioni kutoka kwa mmoja wa wafugaji wa kijiji cha Mkirigi wilayani Kaliua.
Hatua ya kufikishwa mahakamani kwa polisi hao kunakuja wiki chache baada ya gazeti la Mwananchi kuripoti tukio hilo ambapo Takukuru pamoja na uongozi wa polisi mkoa wa Tabora uliamua kufanya uchunguzi na kuthibitisha habari zilizoandikwa na Mwananchi.
Waliofikishwa mahakamani leo baada ya kufukuzwa jeshini kuanzia jana ni pamoja John Okinda, Kabila Pius na Patrick Robert, huku mtuhumiwa mmoja, Elisha David akifanikiwa kutoroka muda mfupi kabla ya kukabidhiwa mikononi mwa Takukuru.
Mbele ya hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Urambo, Hassan Momba inadaiwa na wakili wa Takukuru, Edsoni Mapalala kuwa watuhumiwa hao walitenda makosa hayo Machi 7, mwaka huu.
Wakili Mapalala ameiambia mahakama kuwa siku hiyo katika Kijiji cha Mkirigi kata ya Ilege wilayani Kaliua, washtakiwa wakiwa ni waajiriwa wa Jeshi la polisi waliomba rushwa ya Sh3 milioni kutoka kwa Dotto Ng'andulanye ili wasimchukulie hatua za kisheria baada ya kumtuhumu kumkuta ameotesha mche mmoja wa bangi shambani kwake.
Katika shtaka la pili washtakiwa walidaiwa kupokea rushwa ya Sh3 milioni kutoka kwa Ng'andulanye kama kishawishi cha kutomchukulia hatua za kisheria kitendo ambacho ni kinyume cha sheria.
Watuhumiwa wote wamekana mashitaka dhidi yao na shauri hilo kuahirishwa hadi Aprili 27, mwaka huu itakapoanza kusikilizwa baada ya upande wa mashtaka kuieleza mahakama kuwa upelelezi umekamilika.
Upande wa mashtaka haukuwa na pingamizi kuhusu dhamana ambapo mahakama ilimtaka kila mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili wa kuaminika, mmoja akiwa mtumishi wa Serikali watakaosaini hati ya dhamana ya Sh2 milioni kila mmoja.

No comments :

Post a Comment