dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, April 16, 2016

Rais Magufuli azindua ujenzi wa barabara ya juu Dar Es Salaam!

Mh.Pro. Mbarawa akielezea mikakati ya kujenga na kuboresha miundombinu mbalimbali katika jiji la Dar es salaam.

Rais Magufuli akiongea na wananchi kabla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara za juu na kutaka mradi huo ukamilike haraka.

Rais Magufuli aeleza namna vijana watakavyonufaika na mradi huu wa ujenzi wa barabara za juu.

Hii hapa kauli ya rais magufuli juu ya mpango wa kupunguza msongamano wa magari kwa jiji la Dar es Salaam.



By Matern Kayera, Mwananchi Digital
Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli ameweka jiwe la msingi kwa ajili ya kuanza  rasmi ujenzi wa barabara ya juu kwenye makutano ya barabara za Nyerere na Mandela eneo la Tazara jijini Dar es Salaam leo.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Rais Magufuli amesema ujenzi huo wa barabara ya juu utaanza mara moja kwa ushirikiano na serikali ya Japan  na utagharimu Shilingi 100 bilioni. Amesema, serikali ya Japan imefadhili mradi huo kwa Sh 93.44 bilioni wakati serikali ya Tanzania imechangia Sh 8.36 bilioni.
Rais amewataka wananchi watakaopata ajira kwenye ujenzi wa mradi huo wawe waaminifu na wasiwe wezi wa mafuta, vifaa vya ujenzi au kuendekeza migomo.
“Pia serikali ya awamu ya tano imetenga Sh 1 trilioni kuanza ujenzi wa reli ya kisasa (standard gauge) kwa reli ya kati. Tutajenga kituo kikubwa Ruvu ili mizigo isafirishwe kwa njia ya reli kutoka bandari ya Dar es Salaam hadi Ruvu na malori yatakuwa yakichukua mizigo pale, jambo hili litasaidia kupunguza foleni hapa Dar es Salaam,” alisema Rais Magufuli.
Aidha ameishukuru serikali ya Japan kwa ufadhili wa miradi ya maendeleo nchini kwa zaidi ya miaka 36. Amesema Japan imekuwa ikiisaidia Tanzania bila masharti kama ilivyo kwa baadhi ya wafadhili wa maendeleo. Akionyesha kukerwa na wafadhili wanaotoa misaada yenye masharti na vitisho, Rais Magufuli amesema“Ni bora kula muhogo wa kujitafutia kuliko kula mkate kwa masimango.”
Mbali na mradi huo, Rais amesema serikali yake pia itajenga barabara ya njia sita kutoka Dar es Salaam hadi Chalinze ambayo itakuwa na barabara za juu tano.
Pia amewataka Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda, Wakuu wa Wilaya na Mameya kuhakikisha jiji la Dar es Salaam linakuwa safi muda wote na wachafuzi wa mazingira wachukuliwe hatua za kisheria.

No comments :

Post a Comment