Top Leaderboard Advert

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Zanzibar Diaspora

High class shops @ Fuoni

High class shops @ Fuoni

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Adsense Marquee

Monday, April 11, 2016

Sherehe za Kuapishwa Mawaziri na Manaibu Wao Ikulu Zanzibar jana tarehe 10-4-2016

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwasili katika viwanja vya Ikulu huhudhuria hafla ya kuapishwa kwa Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar leo asubuhi Ikulu Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwasili katika viwanja vya Ikulu kwa ajili ya zoezi la kuwaapisha Mawaziri baada ya kuwateuwa hivi karibuni Hafla hiyo imefanyika katika Viwanja vya Ikulu Zanzibar.
Viongozi wa Serikali wakihudhuria hafla ya kuapishwa kwa Mawaziri Ikulu leo.wa kwanza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid na Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu.
Viongozi wa Serikali na Dini wa kwanza Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe Said Hassan Said na Kadhi Mkuu wa Zanzibar Shekh Khamis Haji Khamis wakihudhuria hafla hiyo Ikulu leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimuapisha Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Zanzibar Balozi Amina Salum Ali Ikulu Zanzibar leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akitia saini Hati ya Kiapo ya Mhe Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Mhe Amina Salum Ali.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimuapisha Waziri wa  Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Haroun Ali Suleiman.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimpongeza Mhe Haroun Ali Suleiman baada ya kula kiapo cha Utii.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimuapisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Mohammed Aboud Mohammed.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akitia saini Hati ya Kiapo ya Mhe Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Mohammed Aboud Mohammed. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimuapisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Mhe Haji Omar Kheri.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akitia saini Hati ya Kiapo ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Mhe. Haji Omar Kheri
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimuapisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe Issa Haji Ussi Gavu. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akitia saini Hati ya Kiapo ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Issa Haji Ussi Gavu. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimuapisha Waziri wa Afya Zanzibar Mhe Mahmoud Thabit Kombo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akitia saini Hati ya Kiapo ya Waziri wa Afya Mhe Mahmoud Thabit Kombo. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimuapisha Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Mhe Balozi Ali Abeid A.Karume.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akitia saini Hati ya Kiapo ya Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Mhe Balozi Ali Abeid A.Karume.
Mhe Hamad Rashid Mohamed akielekea Jukwaa Kuu la kuapishwa kwa ajili ya kula kiapo cha Utii.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimuapisha Waziri wa Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Mhe Hamad Rashid Mohamed.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akitia saini Hati ya Kiapo ya Waziri wa Kilimo Maliasili Mifungo na Uvuvi Mhe Hamad Rashid Mohamed.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimuapisha Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe Dk Khalid Salum Mohammed.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akitia saini Hati ya Kiapo ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe Dk Khalid Salum Mohammed.
Mhe Moudline Castico akielekea katika Jukwaa Maalum la kuapi katika Viwanja vya Ikulu Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimuapisha Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Vijana Wanawake na Watoto Mhe Moudline Castico.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akitia saini Hati ya Kiapo ya Mhe Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Vijana Wanawake na Watoto Mhe Moudline Castico.
Mhe Rashid Ali Juma akielekea katika Jukwaa Maalum lililoandaliwa kwa ajili ya hafla ya kuapishwa Mawaziri Ikulu Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimuapisha Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Mhe Rashid Ali Juma.
Mhe Riziki Pembe Juma akielekea katika Jukwaa Kuu kwa ajili ya kula kiapo cha Utii wakati wa hafla hiyo iliofanyika katika Viwanja vya Ikulu Zanzibar leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimuapisha Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Riziki Pembe Juma.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimuapisha Waziri wa Ardhi,Maji,Nishati na Mazingira Mhe Salama Aboud Talib. 
Mhe Juma Ali Khatib akielekea katika Jukwaa maalum kwa ajili ya kula kiapo cha Utii kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimuapisha Waziri Asiyekuwa na Wizara Maalum na Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi Mhe Juma Ali Khatib, hafla hiyo imefanyika katika Viwanja vya Ikulu Zanzibar.
Mhe Said Soud Said akielekea katika jukwaa maalum kwa ajili ya kula kiapo cha Utii.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimuapisha Waziri Asiyekuwa na Wizara Maalum na Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi Mhe Siad Soud Said hafla hiyo imefanyika katika Viwanja vya Ikulu Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akimpongeza Mhe Waziri Asiyekuwa na Wizara Maalum Mhe Siad Soud Said, baada ya kumaliza kuapa wakati wa hafla hiyo iliofanyika leo katika viwanja vya Ikulu Zanzibar.
Mhe Harusi Said Suleiman akielekea katika Jukwaa Maalum la kuapia katika Viwanja vya Ikulu Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimuapisha Naibu Waziri wa  Afya Zanzibar Mhe Harusi Said Suleiman.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akitia Saini Hati ya Kiapo ya Mhe Harusi Said Suleiman.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimuapisha Naibu Waziri wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Mhe Chuom Kombo Khamis.   
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisaini Hati ya Kiapo ya Mhe Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Mhe Choum Kombo Khamis. 
Mhe Khamis Juma Maalim akielekea katika Jukwaa Maalum la kuapia katika Viwanja vya Ikulu Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimuapisha Naibu Waziri wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Khamis Juma Maalim. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisaini Hati ya Kiapo ya Mhe Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora Zanzibar Mhe Khamis Juma Maalim.
Mhe Juma Makungu Juma akielekea katika Jukwaa Maalum lililoandaliwa kwa ajili ya hafla ya kiapo cha Mawaziri Ikulu Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimuapisha Naibu Waziri wa  Wizara ya Ardhi Maji Nishati na Mazingira Mhe Juma Makugu Juma.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimuapisha Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Mhe Lulu Msham Abdalla. 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimuapisha Naibu Waziri wa  Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Mmanga Mjengo Mjawiri.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimuapisha Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi Mawasiliani na Usafirishaji Mhe Mohamed Ahmad Salum.

Mawaziri Wateule wa Baraza la Mapinduzi la Mawaziri wa Zanzibar wakipitia hati zao za kiapo kabla ya kuaza kwa zoezi hilo lililofanyika katika Viwanja vya Ikulu Zanzibar leo asubuhi.
Waheshimiwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakiwa katika viwanja vya Ikulu Zanzibar wakihudhuria hafla ya kuapishwa kwa Mawaziri Wapya.
Waheshimiwa  Mawaziri Wateule wasio kuwa na Wazira Maalum wakisubiri kula kiapo wa kwanza Mhe Siad Soud Said wa Chama cha AFP na Mhe Juma Ali Khatib wa Chama cha ADA-TADEA wakisubiri kula kiapo leo asubuhi.
Wanafamilia wakihudhuria hafla ya kuapishwa kwa Mawaziri katika Viwanja vya Ikulu Zanzibar leo asubuhi.
Waheshimiwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakiwa katika viwanja vya Ikulu wakihudhuria hafla ya kuapishwa kwa Mawaziri. 
Viongozi wa Serikali na Vikosi vya Ulinzi na Usalama Zanzibar wakishiriki katika hafla ya kuapishwa Mawaziri katika Viwanja vya Ikulu Zanzibar.
Mawaziri Wateule wakisubiri zoezi la kula kiapo katika Viwanja vya Ikulu Zanzibar.
Makatibu Wakuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakihudhuria hafla ya kuapishwa kwa Mawaziri Zanzibar katika Viwanja vya Ikulu Zanzibar.
Wageni waalikwa wakihudhuria hafla ya kuapishwa kwa Mawaziri hafla iliofanyika katika viwanja vya Ikulu Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Manaibu Mawaziri wa Wizara mbali mbali (waliosimama) pamoja na Viongozi Wakuu baada ya kuwaapisha Wajumbe wapya wa Baraza la Mawaziri kwa kipicha pili cha Uongozi wake   katika hafla ya kuapisha Baraza jipya la Mawaziri iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu, [Picha na Ikulu.]

Baraza la Mawaziri Lililoapishwa Leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein Ikulu Zanzibar.

 Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Mhe,Hamad Rashid. Mohamed 
 Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Mhe,Balozi Amina Salum Ali.
 Waziri asiyekua na Wizara Maalum Mhe Soud Said Soud
 Waziri Asiyekua na Wizara Maalum Mhe Juma  Ali Khatib.
 Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira –  Mhe. Salama Aboud Talib.
 Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe,Riziki Pembe Juma.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Issa Haji Ussi Gavu
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe,Mohameed Aboud Mohammed
 Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo – Mhe. Rashid Ali Juma
 Waziri wa Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto Mhe, Moudline Castico.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria Utumushi wa Umma na Utawala Bora Mhe,Haroun Ali Suleiman.
 Waziri wa Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji Mhe,Balozi Ali Abeid Karume.
 Waziri wa Afya - Mhe. Mahmoud Thabit Kombo.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Idara


  Maalum za SMZ -  Mhe. Haji Omar Kheri.
 Waziri wa Fedha na Mipango – Mhe. Dkt. Khalid Salum
   Mohammed
 Naibu Waziri wa Afya- Mhe. Harusi Said Suleiman
 Naibu Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo -   Mhe. Bibi Chum Kombo Khamis.
 Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora - Mhe.  Khamis    Juma Maalim.
Naibu Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi -    Mhe. Lulu Msham Abdulla
Naibu Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira      Mhe. Juma Makungu Juma.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Mmanga Mjengo Mjawiri.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji - Mhe. Mohammed Ahmad Salum.

Dk Awaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri Ikulu leo


 
STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar                                     10.4.2016
---
RAIS wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein leo amewaapisha Mawaziri na Manaibu Mawaziri wa Wizara 13 za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Mawaziri wasiokuwa na Wizara Maalum ambao pia ni Wajumbe wa Baraza la Mapinduzi.

Hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya Ikulu mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa vyama na Serikali pamoja na wananchi kadhaa ambapo miongoni mwa waliohudhuria ni Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu, Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zubeir Ali Maulid.

Wengine ni Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe. Said Hassan Said, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji na Mkuu wa  Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Abdalla Mwinyi Khamis. Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar Khatib Abrahman Khatib pamoja na viongozi wa vikosi vya Ulinzi.


Walioapishwa katika hafla hiyo ni Waziri, Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Issa Haji  Ussi Gavu, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora  Mhe. Haroun Ali Suleiman. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ   Mhe. Haji Omar Kheri, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Mohammed Aboud Mohammed.  

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Khalid Salum Mohammed, Waziri wa Afya Mhe. Mahmoud Thabit Kombo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Riziki Pembe Juma pamoja na Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Mhe. Moudline Castico.

Wengine ni Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Mhe. Balozi Amina Salum Ali, Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Mhe. Balozi Ali Abeid A. Karume. Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Mhe. Hamad Rashid Mohammed. Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Mhe. Rashid Ali Juma na Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Mhe. Salama Aboud Talib.

Kwa upande wa Manaibu Waziri ni Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Khamis Juma Maalim. Naibu Waziri wa Afya Mhe. Harusi Said Suleiman na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Mhe. Mmanga Mjengo Mjawiri.

Wengine ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Mhe. Mohammed Ahmed Salum. Naibu Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo nan Uvuvi Mhe. Lulu Msham Abdulla, Naibu Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Mhe. Bibi Choum Kombo Khamis na Naibu Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Mhe. Juma Makungu Juma.
         
Aidha, Dk. Shein amewaapisha Wajumbe wa Baraza la Mapinduzi na Mawaziri Wasiokuwa na Wizara Maalum akiwemo Mhe. Said Soud Said kuwa Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri Asiekuwa na Wizara Maalum pamoja na Mhe. Juma Ali Khatib Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri Asiekuwa na Wizara Maalum.

Kwa uwezo aliopewa chini ya Vifungu 42, 43,44 na 47 vya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, Dk. Shein ameunda Wizara 13 za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kuwateua Mawaziri na Manaibu Mawaziri wa Wizara hizo pamoja na Mawaziri Wasiokuwa na Wizara Maalum na Wajumbe wa Baraza la Mapinduzi.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 
 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

No comments :

Post a Comment