Top Leaderboard Advert

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Zanzibar Diaspora

High class shops @ Fuoni

High class shops @ Fuoni

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Adsense Marquee

Sunday, April 10, 2016

Simu feki zaacha vilio Kariakoo

By Jackline Masinde na Kalunde Jamal, Mwananchi 
Dar es Salaam. Ni kilio kwa wafanyabiashara wa simu za mkononi katika maeneo ya Kariakoo, Tandika na mengine ya kibiashara nchini baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano (TCRA) kutangaza kuzima simu feki za mkononi kuanzia Juni 16, mwaka huu.
Tamko la TCRA huenda likasababisha asilimia 80 ya simu zilizoko sokoni katika maeneo hayo kugeuka ‘matoi’ ya kuchezea watoto.
Mwananchi iliweka kambi kwenye eneo la kibiashara linalouza simu kwa wingi la Kariakoo na Tandika na kuzungumza na wafanyabiashara hao na kubaini kuwa nane kati ya 10 ya simu zinazouzwa ni feki ambazo kwa sasa wamesema hazitoki tena.
Wafanyabiashara hao walisema tangu Serikali ilipotangaza kuzizima simu hizo wateja wamepungua kwa kiwango kikubwa.
Wafanyabiashara hao walisema tangu Serikali ilipotangaza kuziima simu hizo, wateja wamepungua kwa kiwango kikubwa.
Mmoja wa wafanyabiashara hao, Rehema Mohamed alisema wanalazimika kuuza simu kwa bei ndogo zaidi ili ziishe kabla ya siku ya kuzifungia, lakini pamoja na hilo bado wateja ni wachache.
Mohamed alisema simu za kawaida zilizokuwa zikiuzwa kwa Sh40,000 hivi sasa wanaziuza kwa Sh35,000 hadi 30,000.
Kwa upande wa simu zenye ‘memory card’, intaneti, redio na programu nyingine zinauzwa kwa Sh50,000 badala ya Sh80,000 hadi Sh200,000 ya zamani.
“Mara ya mwisho nilileta mzigo wa simu 5,000, kati ya hizo nimeuza 30 tu,” alisema Charles Odemba.
Odemba alisema anatamani mwezi Juni ufike mapema ili ajue mustakabali wa biashara hiyo kwa kuwa hajui atakakozipeleka simu hizo iwapo zitakuwa ni feki.
Omari Juma ambaye pia ni mfanyabiashara sokoni hapo alisema ana simu za thamani ya Sh50 milioni zilizoingia siku moja kabla ya TCRA kutangaza kuzifungia feki na katika mzigo huo ameuza 15.
Kwa upande wake, Valesh Solanki alisema, “Hii ni kiboko ya matapeli, tunaouza simu orijino tutapata soko na heshima itarudi.”
Hamis Massawe ameishauri Serikali kushusha bei ya simu orijino ili kuendana na hali halisi ya kipato cha Watanzania.
TCRA inasemaje?
Meneja wa Mawasiliano wa TCRA, Innocent Mungy alisema wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi namna ya kuzitambua simu bandia na kuwataka kuendelee kufanya ukaguzi wa simu zao.
“Lengo la kuzima simu hizo ni kudhibiti vifaa vya mawasiliano, hususan simu za kiganjani ambavyo havikidhi viwango vya matumizi,” alisema.
“Wanaosema watapata hasara, hao ndiyo hatuwataki maana kama kweli wewe ni mfanyabishara halali kwa nini uuze simu feki?”.
Pia, alisema lengo ni kudhibiti wizi na iwapo mtu atapoteza au kuibiwa simu ya kiganjani na kutoa taarifa kwa mtoa huduma, simu hiyo itafungwa ili isiweze kutumika kwenye mtandao mwingine.
Ofisa Uhusiano wa Shirika la Viwango nchini (TBS), Roida Andusamile alisema: “huwezi kufahamu bidhaa feki hadi uipime, hivyo kama hatujapima ni vigumu kusema kwa sababu zipo feki moja kwa moja na zenye ubora hafifu.”
Ofisa Mwandamizi wa Mawasiliano wa Tume ya Ushindani (FCC), Frank Mdimu alisema suala la simu feki wanalifanyia kazi kwa ushirikiano na TCRA, kwa kutoa elimu kwa wananchi kabla ya kuchukua hatua.

No comments :

Post a Comment