Top Leaderboard Advert

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Zanzibar Diaspora

High class shops @ Fuoni

High class shops @ Fuoni

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Adsense Marquee

Saturday, April 9, 2016

SUA kubuni miwani ya kugundua wadudu, magonjwa yanayoshambulia mimea

By Kalunde Jamal, Mwananchi
Dar es Salaam. Huenda  changamoto katika kilimo zikapata mwarobaini baada ya Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine  (SUA) kubuni miwani maalumu kwa ajili ya kugundua magonjwa na wadudu wanaoshambulia mimea shambani.
Leo, Mchumi wa Kilimo wa Kilimo kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine, Dk Anna Temu alisema miwani hiyo itawawezesha wakulima kuona wadudu na magonjwa yanayoshambulia mimea katika hatua za mwanzo.
Alisema miwani hiyo inayotambulika kitaalamu kama 'Agro Spectacles' itasaidia kuondoa tatizo linalowakabili wakulima wa Tanzania la kufahamu uharibifu wa mazao unapokuwa umekomaa  iwapo tu fedha za kukamilisha wazo hilo zitapatikana.
“Miwani hii inaweza kuhakikisha ongezeko la mavuno ya mazao na hivyo kuboresha usalama wa chakula kwa nchi na mapato ya jumla kwa wakulima, ”alisema Dk Temu.
Akizungumzia changamoto ya kifedha, Dk Temu alisema inakwamisha miradi mingi ya tafiti ikiwamo  masuala ya kilimo.
Akizungumza katika warsha hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa  Tume ya Sayansi na Teknolojia, (Costech) DkHassan Mshinda aliwaomba wafadhili na Serikali kuongeza fedha za kufanyia tafiti ili kusaidia masuala mbalimbali ya maendeleo ikiwamo ya kilimo, biashara.

No comments :

Post a Comment