dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, April 5, 2016

Tajiri wa Kiarabu atua African Lyon

  • Bilionea wa Kiarabu, Dk Sulaiman Al-Fahim ametangazwa kuwa mwenyekiti mtendaji wa klabu ya African Lyon itayoshiriki Ligi Kuu Bara msimu ujao.


Mmiliki wa klabu ya African Lyon, Rahim Kangezi alisema kuwa waliamua kumuomba Al Fahim kuwa kushika nafasi hiyo kutokana na uzoefu wake katika michezo hasa soka.

Kangezi alisema kuwa Al Fahim ni Rais wa kampuni ya Arab Union for Real Estate Development ya Dubai na miaka ya nyuma alikuwa msemaji wa kampuni inayomiliki klabu tajiri duniani, Manchester City, Abu Dhabi United Group (ADUG). ADUG iliinunua Manchester City mwaka 2008.

Pia Al Fahim alitaka kununua klabu ya Portsmouth wakati ikishiriki Ligi Kuu England kabla ya mpango huo kushindikana.


Kangezi alisema kuwa Al Fahim ataanza kazi rasmi Aprili 16.


Alisema kuwa uwepo wa Al Fahim kuitaifanya timu hiyo kuwa na uongozi bora wenye kujua uendeshaji wa kisasa katika masuala ya soka kwa kuzingatia uzoefu wa mfanyabiashara huyo.

“Haikuwa kazi rahisi Al Fahim kukubali kuingia kwenye uongozi wa klabu yetu, ila tunashukuru kwani alituelewa baada ya kukutana naye alipokuja hapa nchini kwa shughuli zake, “ alisema Kangezi.

Alisema kuwa lengo lake ni kuona African Lyon inakuwa klabu ya mfano sit u kwa Tanzania, hata kwa nchi za Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla. Kangezi alisema kuwa mipango yao ya awali ni kuhimarisha timu ya kwanza ili iweze kufanya vyema katika mashindano ya ligi kuu na pia kuanzisha msingi mzuri wa timu za watoto.

“Dk Sulaiman ni Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa kampuni ya Al Fahim Group na vile vile alikuwa mkurugenzi wa kituo cha Royal Football Fund (RFF) mbali ya kuwa mchezaji wa mchezo wa chesi, ameahidi kusaidia wachezaji chipukizi ili kuwawezesha kushiriki katika mpira wa kulipwa, tunaamini titafika, ” alisema.

No comments :

Post a Comment