dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, April 6, 2016

Ufisadi wa Sh. bilioni 37 waibuliwa Jeshi la Polisi

  • KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), imeibua kashfa ya ufisadi wa mabilioni ya fedha ndani ya Jeshi la Polisi nchini.





Mkataba huo unalihusisha jeshi hilo na kampuni ya Lugumi Enterprises Limited ambao uliingiwa mwaka 2011 kwa kazi ya kufunga mitambo ya kuchukua alama za vidole katika vituo vyote vya polisi nchini.

Katika mkataba huo wenye gharama ya Sh. bilioni 37, Lugumi Enterprises Limited ilipewa kazi ya kufunga mitambo hiyo katika vituo 108 lakini hadi sasa imefunga katika vituo 14 tu.

Mbali na kufanya kazi hiyo kwa kiwango kidogo, kampuni hiyo imeshalipwa Sh. bilioni 34 takiwa ilipa siku sita Jeshi la Polisi nchini kupeleka mkataba kati yake na Kampuni ya Lugumi Enterprises wa gharama ya Sh. bilioni 37 kwa ajili ya kufunga mitambo ya alama za vidole katika vituo vyote vya polisi nchini.Hatua hiyo inatokana na PAC kutoridhishwa na maelezo yaliyotolewa na Jeshi la Polisi juu ya mkataba huo ulioingiwa mwaka 2011, ambao kampuni hiyo imeshalipwa Sh. bilioni 34, ambazo ni takriban asilimia 92.

Kutokana na utata wa mkataba huo na utekelezaji wake, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), imeliagiza Jeshi la Polisi kuwasilisha mkataba huo ndani ya siku sita kuanzia jana.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Hilaly Aeshi, alisema jana kuwa Kamati yake imeshtushwa na taarifa hiyo, jambo ambalo limesababisha kuwapo maswali mengi.

“Haya tumeyabaini baada ya kamati kukutana na watendaji wa Jeshi la Polisi, ambao waliwasilisha taarifa namna wanavyotunza mali za serikali pamoja na wanavyotumia fedha,” alisema.

Alisema kamati yake imeshtushwa kusikia kuwa kampuni hiyo ilishalipwa karibu fedha zote kulingana na mkataba, lakini hadi sasa kazi hiyo haijamalizika na imefanyika katika mkoa wa Dar es Salaam tu.

“Tumewaomba waje Aprili 11, watuletee mkataba huo tuuone kwa sababu haiwezekani tangu mwaka 2011 hadi leo kampuni hiyo iwe imefunga mashine katika vituo 14 tu wakati fedha wameshalipwa,” alisema Aeshi.

Alisema Kamati imetoa maagizo mengine kwa Jeshi la Polisi, ikiwamo kuundwa kwa timu maalumu ya ukaguzi, itakayojumuisha ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ili kukagua mali za wananchi zinazokuwapo katika vituo vya polisi kwa muda mrefu pamoja na ukaguzi wa mizigo bandarini ufanywe na jeshi hilo badala ya kampuni binafsi.

“Utakuta mizigo ya jeshi inashushwa bandarini kwa kuwa hailipiwi kodi wala kukaguliwa basi inaruhusiwa tu bila kujua ndani kuna nini. Hali hiyo inatumiwa na wajanja kupenyeza mizigo yao ndani ya mizigo ya jeshi,” alisema Aeshi.

Naye Mkuu wa Jeshi la Polisi nchi, Inspekta Jenerali (IGP), Ernest Mangu, alisema kwa sasa jeshi la polisi linashughulikia ujenzi wa nyumba za askari nchi nzima.

Alisema serikali imeingia mkataba na kampuni nyingi nchini za ujenzi wa nyumba hizo na kwamba limeanza kuboresha utendaji kazi ili liwe karibu na wananchi.

“Lengo ni kuondoa kero zilizopo kwa wananchi. Hii programu tunayotaka kuianzisha tutaizindua Juni na baadaye itaendelea katika mikoa mingine, hivyo jeshi la polisi tumejipanga,” alisema Mangu.

Alisema taarifa za ukaguzi wa fedha katika jeshi la polisi katika mwaka wa fedha uliopita ulikuwa mzuri.

/NIPASHE

No comments :

Post a Comment