Top Leaderboard Advert

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Zanzibar Diaspora

High class shops @ Fuoni

High class shops @ Fuoni

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Adsense Marquee

Thursday, April 7, 2016

Uteuzi wa Dk. Shein wakosolewa Zanzibar

HATUA ya Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, kuteua viongozi watatu wa vyama vya upinzani kuwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi (BLW), imeelezwa kuwa itasadia kupuguza joto la siasa lakini haitomaliza mpasuko wa kisiasa visiwani hapa.

Mtazamo huo umetolewa na wananchi mbalimbali katika Manispaa ya Mji wa Zanzibar, walipohojiwa na Nipashe kwa nyakati tofauti, siku mbili tangu kufanyika kwa uteuzi huo.
Viongozi waliteuliwa kuwa wajumbe wa BLW ni Hamad Rashid Mohamned (ADC), Juma Ali Khatib (TADEA) na Soud Said Soud (AFP). Wote walikuwa wagombea wa urais katika uchaguzi wa marudio, uliofanyika Machi 20, mwaka huu.
Nuru Kassim Islam, mkazi wa Mkunazini alisema uteuzi uliofanyika utasadia Baraza kuonekana kuwa na wajumbe wa upinzani lakini mpasuko wa kisiasa utaendelea kwa sababu viongozi walioteuliwa hawaungwi mkono na wananchi wengi visiwani.
Alisema mpasuko wa kisiasa ulikuwa umemalizika baada ya kuundwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) kwa sababu vyama vya vya CCM na CUF ndivyo vinavyoungwa mkono na wananchi wengi Zanzibar.
Hata hivyo, alisema baadhi ya viongozi wa CCM walikuwa na kinyogo na SUK, ndiyo maana imeshindwa kuendelea na kuirudia nyuma siasa za chuki na uhasama.
“Tangu mwanzo, viongozi wa CCM baadhi yao hawakuitaka serikali ya umoja wa kitaifa na sasa wamefanikiwa kuivunja.
Lakini nchi kuendelea si jambo la Rais kama Wazanzibari hawawezi kukaa pamoja na kutafuta suluhu,” alisema.
Suleiman Ali Mohamed, mkazi wa Mkunazini alisema pamoja na kufanyika uteuzi huo, lengo la kuwaunganisha Wazanzibari haliwezi kufanikiwa bila kupatikana muafaka kati ya CCM na CUF.
Alisema viongozi walioteuliwa walikataliwa na Wazanzibari ndiyo maana serikali ya umoja wa kitaifa imekwama kuundwa kutokana na vyama vyao kushindwa kufikia masharti ya Katiba ya Zanzibar.
“Mpasuko wa kisiasa utaendelea kuwapo kwa sababu viongozi walioteuliwa hawana nguvu za wanachi. Watasadia Baraza kuwa na watu wenye itikadi tofauti lakini hawana ubavu wa kumaliza mgogoro wa uchaguzi wa Zanzibar,” alisema Suleiman, maarufu kama Sukari.
Wakizungumzia ahadi ya Rais Dk. Shein ya kupambana na rushwa na ufisadi pamoja na uwajibikaji kwa viongozi na watendaji wakuu, walisema bado wana wasiwasi na utekelezaji wake
Abubakari Pandu Mjaja alisema kama Rais alikuwa na nia ya kupambana na rushwa na ufisadi, alitakiwa kuchukua hatua tangu mwaka 2010 alipoingia madarakani.
Mjaja alisema rushwa na ufisadi Zanzibar limekuwa tatizo sugu na hakuna watu wanaochukuliwa hatua licha ya kuundwa kamati teule za uchunguzi za Baraza la Wawakilishi, ikiwamo malipo ya mishahara hewa, ufisadi wa majengo ya serikali na ardhi.
Asha Hamad Hassan, mkazi wa Kwahani, alisema kabla ya Rais kuanza kutumbua majipu, viongozi na watendaji watakaokuwa ndani ya serikali au nje, wachuguzwe mali wanazomiliki na watakaobainika kumiliki kwa njia chafu wachukuliwe hatua.
Aidha walisema kabla ya Rais kupambana na rushwa na ufisadi, achukue hatua za kuondoa tatizo la dawa za kulevya, linaloendelea kuvuruga nguvu kazi ya vijana.
Akizindua Baraza la Wawakilishi juzi, Dk. Shein alisema mwelekeo wa serikali yake utakuwa kupambana na rushwa na ufisadi pamoja na kujenga msingi wa uwajibikaji kwa viongozi na watumishi wa umma.

No comments :

Post a Comment