dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, April 8, 2016

Vita ya Makonda, Meya wa Ukawa inavyoanza kuchemka

  • KATIKA kile kinachoonekana kuwapo kwa ‘mpambano’ kati ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, na Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita, dalili zimeanza kuonekana kutokana na vita ya maneno kati yao.



Hatua hiyo imeonekana baada ya viongozi hao wawili wa serikali kuu na mamlaka ya serikali za mitaa, kwa nyakati tofauti kutoa kauli zinazokinzana, hali inayoashiria mbele ya safari hali haitakuwa shwari.

Mwita, ambaye mwishoni mwa wiki iliyopita alipohojiwa na Nipashe alisema atakuwa tayari kushirikiana na Paul Makonda, alitoa sharti kwamba atafanya hivyo iwapi mteule huyo wa Rais atakuwa na lengo la kuleta maendeleo na si kufanya siasa.

Kauli hiyo ya Mwita imeonekana kama vile ‘kujibu mapigo’ ya kauli ya Makonda aliyoitoa hivi karibuni, alipozungumza na baadhi ya waendesha bodaboda wa Dar es Salaam kwamba: “Mamlaka ya uamuzi ya utendaji kazi Mkoa wa Dar es Salaam yako mikononi mwangu. Wengine wataishia kusema wee, lakini mwenye mamlaka ya mwisho katika uamuzi ni mimi.”

Kauli hizo kizani ndizo hasa zinazoonyesha kuanza kwa vita ya maneno kati ya Isaya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), anayetokana na mwavuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), dhidi ya Makonda ambaye ni kada wa CCM na kwa muda mrefu amekuwa akikwaruzana na upinzani.

Matumaini ya Mwita
Akizungumzia ushirikiano wake na Makonda, Mwita alisema: “Sikuja kufanya siasa hapa. Tangu awali nilisema nimekuja kuleta maendeleo ya wana Dar es Salaam, suala la siasa tuweke kando, tuwahudumie wananchi ambao wako wenye itikadi za vyama na wasio na vyama.

“Suala la siasa itafika wakati tutafanya. Yeye kama anawajibika kwa Rais afanye, ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa atekeleze majukumu yake. Nitaendelea kumuunga mkono kwenye mambo ya msingi ili taifa letu lipige hatua.

Alitolea mfano wa mambo ya msingi ya kuungana kuwa ni pamoja na jitihada za mkuu huyo wa mkoa, kuhakikisha Jiji linakuwa safi.

“Nina majukumu ambayo kimsingi natakiwa kuyafanya, naye ana yake. Tukianza kunyooshena vidole na nisingependa ifike huko bali tufanye kazi kwa pamoja ili taifa letu na Dar es Salaam kwa ujumla ipate maendeleo,” alisisitiza.

“Ukimchukua Makonda kama Makonda nani anajua ni mwanasiasa nami huwezi kunijua kwa kuniangalia, hivyo tujenge taifa letu sote. Nachotaka ni maendeleo na nitafurahi sana kama tutaungana kuwaleta Watanzania maendeleo kuliko maslahi yetu ya kisiasa kutangulia mbele,” alibainisha.

Aliyataja baadhi ya mambo kuwa ni pamoja na watoto wengi wa shule za msingi na sekondari jijini kukaa chini kwa kukosa madawati ya kukalia, mawasiliano ya barabara kukatika, ukosefu wa barabara na huduma za maji na kwamba yote hayo yatafanikiwa kwa kuweka kando siasa.

Meya huyo ambaye alisisitiza kuwa hakuja kununuliwa bali kufanya kazi, alisema kipaumbele chake ni kufanya kazi kwa kuwa aliomba kufanya kazi.

Meya huyo ambaye pia Diwani wa Kata ya Vijibweni, alisema kabla ya kupata nafasi hiyo hakuelewa uzito wake, lakini kwa sasa anajisikia ana deni na mzigo mzito.

“Kuna mambo matatu ambayo ni matarajio ya Watanzania kwa kiti nilichokalia. Kwanza nitoe majibu sahihi, pili nisipoteze uhusiano mzuri na tunaofanya nao kazi, na tatu kutimiza mambo ya msingi ya kimaendeleo,” alisisitiza.

Usafi

Akizungumza mikakati ya kuhakikisha Dar es Salaam inakuwa safi, Mwita alisema yeye na wenzake watahakikisha Jiji linakuwa safi muda wote na mkakati wa kwanza ni kuanzisha madampo katika wilaya zote badala ya kutegemea lile la Pungu, kama ilivyo sasa.

“Suala hili linakwenda kwa vikao zaidi nitalipeleka kwenye vikao na wakiona linafaa tutanunua maeneo na kujenga madampo ya kisasa. Inakuwa ngumu sana kutoa takataka Kawe kupeleka Pugu ambako ni zaidi ya kilomita 30. Tungekuwa na dampo kule kule tungepunguza gharama za kuzoa taka,” alisema.

Pia alisema watahamsisha usafi shirikishi kwa kuwa hakuna namna anaweza kufanya bila wao (Watanzania) kuamua kufanya.

Aidha, alisema atakutana na waliopewa zabuni ya kuzoa taka katika mitaa mbalimbali ya Jiji na kupata ushauri na changamoto wanazokutana nazo, kiasi cha kushindwa kuzoa taka.

“Hatuwezi kufanikiwa bila kuwa na madampo kila wilaya. Tunataka tuwe na madampo ya kisasa ambayo hayatakuwa kero kwa wananchi. Tutatumia bajeti zetu kutekeleza hili,” alisema.

Kuhusu matumizi ya takataka kuwa malighafi, alisema wameanza na wilaya ya Kinondoni kuwa na kiwanda cha kuchakata takataka kwa ufadhili wa Manispaa ya Mji wa Humberg, Ujerumani, kitakachojengwa Mabwepande na kwamba viwanda kama hivyo vitajengwa katika manispaa zote kadri wafadhili watakavyopatikana.

Kwa upande wa majitaka, alisema anatambua kuwa miundombinu mingi imechakaa huku idadi ya watu ikiongezeka siku hadi siku na kwamba inahitaji ukarabati mkubwa. Alisema watahakikisha wanalisimamia kikamilifu suala hilo, ikiwa ni pamoja na kuondoa harufu inayojitokeza katika madampo hayo.

“Watanzania wajue hatukuja kutafuta fedha za mifuko yetu bali kufanya kazi. Tutafanya kazi na wataona kweli kazi imefanyika. Ninayoyasema ni lazima yatimie,” alisema.

Juu yac miundombinu ya barabara, alisema ni lazima Watanzania walipe kodi ili kupata fedha za kujenga barabaraba za mitaa ambazo nyingi ziko katika hali mbaya.

“Shida kubwa ni jinsi makandarasai walivyopatikana na kupewa kazi ya ujenzi wa barabara hizo. Tutazijenga barabara zote na katika utekelezaji wa hilo tumeanza kutoa Sh milioni 200 kila kata, ambayo ni sawa na Sh. bilioni nne kwa mwaka huu,” alisema.

Mwita alisema cha msingi ni Watanzania kulipa kodi ambayo itasaidia kuharakisha maendeleo na kwamba kila kitakachokusanywa kitaelekezwa kwenye maendeleo na kutakuwa na mchanganuo wa wazi utakaobandikwa katika mbao za matangazo.

MIPANGO MIJI
Anasema suala la mipango miji ni mtambuka na matamanio yake ni Jiji kuwa na mpangilio sawa kama yalivyo majiji ya Nairibo nchini Kenya na Kampala nchini Uganda.

Alisema licha ya kufanikiwa kwa majiji hayo kimfumo kwa kuwa Meya wa Jiji anachaguliwa na wananchi kwa mamalaka ya mji kuwa chini yake na Jiji la Kampala wana Wizara inayosimamia tofauti na Tanzania ambako madiwani wa halmashauri zote wanapiga kura ya kumchagua Meya.

“Kwa kuwa tuna mameya wawili wanaotokana na Ukawa na wa CCM tutashirikiana. Kuna namna ya kupanga Jiji letu kwenye mpangilio mzuri. Kwa kuwa tutakuwa tunampa mrejesho rais tutasaidia kuhakikisha linakuwa kwenye mpangilio.

Aidha, alisema operesheni kabambe kukabiliana na waliojenga maeneo ya wazi itafanyika kwa kuwa wapo ambao wamejimilikisha na kuwa na hati ya maeneo husika huku katika mipango miji ikionyesha kuwa ilipaswa kuwa eneo la wazi.

“Waliojenga maeneo ya wazi tutasumbuana kidogo, kuna viwanja vya michezo watu wamevamia tutakuwa wakali, wapo wamevamia kwa kujuana na kutengeneza hati miliki hivyo wajue tutasumbuana,” alisisitiza.

MAKUSANYO
Meya huyo alisema ni lazima kampuni na mashirika mbalimbali Jijini kulipo kodi ya huduma ya jiji, kwa kuwa wote wanafanya biashara na kuingiza mapato.

“Tunawahakikishia wakilipa tutakuwa tunawatangaza kwenye vyombo vya habari na tutawapa cheti cha shukrani, kodi hii ni muhimu sana kwa uendeshaji wa Jiji katika huduma muhimu za jamii,” alisema.

/IPPMEDIA

No comments :

Post a Comment