dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, April 6, 2016

Walimu wakimbia vipigo Kondoa!

  • SIKU chache baada ya serikali kulaani kitendo cha kupigwa daktari mkoani Mtwara, wilayani Kondoa, mkoa wa Dodoma, imeelezwa kuwa wananchi wamepiga walimu.











Tukio hilo limepelekea baadhi ya walimu kukimbia kwenye shule wanazopangiwa kufundisha na kusababisha kuwapo kwa uhaba wa walimu wilayani humo.

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, Hussein Ngaga, wakati akizungumza na wananchi katika kijiji cha Kinyasi, wilayani humo kuhusiana na tatizo la ndege waharibifu aina ya Kweleakwelea waliovamia mashamba.

Katika mkutano huo, mmoja wa wananchi hao, Valentino Petro, alisema kijiji chao kina tatizo la walimu kushindwa kukaa kutokana na kukosekana kwa huduma ya maji.“Sisi hapa walimu wanne wameondoka, tunaomba serikali itusaidie kuleta walimu wengine maana hawa wamesema hawawezi kukaa kutokana upatikanaji wa maji kuwa wa shida,” alisema Petro.

Akizungumza, mkurugenzi huyo aliwaambia kuwa hali ya elimu wilayani humo si nzuri kutokana na wananchi kuwa na mahusiano mabaya na kuwapiga walimu.

“Tuwatunze walimu na tutengeneze mahusiano mazuri nao, serikali inajitahidi kuleta walimu lakini nyie mnajenga nao mahusiano mabaya lazima wataondoka, mpaka sasa walimu wanne wameshaondoka hapa kijijini kwenu,” alisema.

Alikitaja kijiji ambacho tukio la kupigwa mwalimu lilitokea hivi karibuni kuwa ni Masange, ambako walimu wawili wa shule ya msingi walipigwa na wakazi wa kijiji hicho.

Ngaga alisema mwaka 2012, Kondoa ilikuwa ya mwisho kwenye mitihani ya kumaliza darasa la saba na walimu wamekuwa wakifanya juhudi ili kuongeza ufaulu, lakini wazazi wanakwamisha.

“Watoto wetu wasiposoma hawatakuwa na nafasi katika hii dunia, huko tunakokwenda inatakiwa shule tu si mambo mengine, kama mtashindwa kuwatunza walimu na kuwapiga, watoto wetu watakosa elimu,” alisema.

Aliwataka wananchi wa Kondoa kushikamana ili kuhakikisha walimu wanaishi katika mazingira rafiki kwa kuwa na mahusiano mazuri nao.

No comments :

Post a Comment