dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, April 10, 2016

WAvamizi wajimilikisha shamba la Sumaye

  • HATIMAYE wavamizi shamba la ekari 33 la aliyekuwa Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, eneo la Mji Mpya, Mabwepande, nje kidogo ya Dar es Salaam, wamejimilikisha rasmi kwa kuweka tangazo linaloelekeza matumizi ya shamba hilo.
Nipashe imefanikiwa kuona tangazo hilo ambalo limeandikwa kwa maneno yenye rangi nyeusi na nyekundu yanayosomeka:
Eneo hili ni la shule, zahanati, eneo la wazi kwa ajili ya wananchi wa Kinondoni ni marufuku kujenga eneo hili asanteni-Wananchi.
Baada ya Nipashe kuona tangazo hilo iliwasiliana na Sumaye juzi ambaye alikiri kufahamu uwapo wa tangazo hilo katika shamba lake na kusema halijawekwa na mamlaka bali wavamizi na kwamba ameanza kuchukua hatua mbalimbali.
“Shamba hili ni mali yangu kwa nini nilisuse, hawa walioweka tangazo kwenye shamba langu ni wavamizi sio mamlaka za serikali, watambue shamba hili ni langu na hatua mbalimbali nimeanza kuchukua, litaendelea kuwa langu,” alisema Sumaye aliyeongoza serikali 1995-2005.
Mwezi Februari, Sumaye aliliambia Nipashe kuwa maamuzi ya shamba lake yapo mikononi mwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Sumaye alitoa kauli hiyo baada ya mwishoni mwa mwezi Januari Makonda kuitisha mkutano Mji Mpya ambapo Sumaye aliutumia kwa kuonyesha wavamizi hao hati za umiliki wa ardhi hiyo yenye ukubwa wa heka 33.
Katika mkutano huo, Makonda aliomba apewe wiki mbili ili kutatua changamoto hiyo ikiwa ni pamoja na kupitiwa sheria za umiliki wa ardhi hiyo kama zilikiukwa lakini hadi sasa hajafanya hivyo.
Aidha, makonda aliwaeleza watu waliojenga kwenye shamba hilo, endapo Sumaye atashinda kisheria kuwa ndiye mmiliki halali wa eneo hilo na hakukiuka sheria ya umiliki, mstaafu huyo angeangalia namna ya kuwasaidia wananchi hao.
Aliwaeleza wavamizi hao kuwa watapata eneo endapo Sumaye atakuwa amekiuka sheria za umiliki ardhi na kwamba kinyume na hapo watamuomba awakatie sehemu ingawa itategemeana na mmiliki husika.
Katika utetezi wake siku hiyo, Sumaye alisema baada ya serikali kubadili matumizi ya ardhi, waliacha kulilima miaka mitatu iliyopita ili kujengwe Chuo Kikuu.
Uvamizi wa ardhi hiyo ulitokea mwishoni mwa mwaka jana ambapo zaidi ya watu 100 waligawana eneo hilo na wengine kujenga nyumba za kudumu za matofali na kuainisha wapi kuwe zahanati, makazi, ofisi na uwanja wa michezo.

No comments :

Post a Comment