dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, April 3, 2016

Waziri akwaa kashfa kutosha kutumbuliwa

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni, huenda akawa Waziri wa kwanza kuliaga Baraza la Mawaziri la Rais wa tano, John Magufuli, baada ya watu kuanza kuhoji kashfa yake ya kughushi umri wake ili awanie uenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM).
 
Kashfa hiyo ilibuliwa na wanachama wenzake mwaka 2010 wakati akiwa Mwenyekiti wa UVCCM, Taifa, na mwishowe ilimng’oa baada ya kuthibitika kuwa ni kweli alidanganya umri wake ili apate sifa ya kuwania kiti hicho. 
 
Katika mjadala ulioibuka hivi karibuni kwenye mitandao ya kijamii, baadhi ya watu wanahoji iweje Rais Magufuli amteue kushika nafasi ya umma mtu ambaye aliwahi kuthibitika kughushi umri wake kwa maslahi binafsi.“Yeye ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Wizara ambayo inahusika moja kwa moja na kukamata na kuwachukulia hatua za kisheria wahalifu, wakiwemo watu walioghushi nyaraka, sasa kama yeye aliwahi kughushi kwanini apewe nafasi ya umma,” alihoji mmoja wa wachangiaji wa mjadala huo kwenye mtandao mmoja wa kijamii na kuongeza:
 
“Haya mambo ndiyo ambayo baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere alikuwa akiyakataa.
 
"Inafahamika fika kwamba mtu ana kashfa halafu anapewa nafasi ya uongozi? Watu watajifunza nini kwa mtu 
 
Masauni alidanganya umri wake ili apate nafasi ya kuwania uenyekiti wa UVCCM mwaka 2008 kutokana na umri wake halisi wakati huo kumnyima fursa ya kuwania nafasi hiyo.
 
Kwa mujibu wa Katiba ya UVCCM wakati huo, mtu anayeshika nafasi ya Mwenyekiti alipaswa kumaliza muhula wake wa miaka mitano kabla ya kuvuka miaka 35, lakini wakati huo Masauni alikuwa tayari na miaka hiyo hivyo kukosa sifa za kuwania nafasi hiyo.
 
Iwapo Masauni angemaliza muhula wake wa miaka mitano bila kusakamwa na hatimaye kujiuzulu, angeachia nafasi hiyo mwaka 2012 akiwa na miaka 39 umri ambao unakinzana na Katiba ya UVCCM inayopendekeza Mwenyekiti astaafu akiwa chini ya miaka 35.
 
Naibu Waziri huyo alifanikiwa kughushi kuonyesha kuwa alizaliwa Oktoba 3, 1979 ingawa baba yake mzazi alipohojiwa alikana mwaka huo uliotajwa na mwanaye kwenye nyaraka zake na kusema alizaliwa Oktoba 3, 1973.
 
Baada ya Masauni kufanikiwa kughushi umri wake watu walianza kufuatilia historia yake na kubaini kuwa alianza shule ya msingi mwaka 1979 hivyo kuhoji iweje mtoto azaliwe mwaka huo huo na aanze shule ya msingi wakati huo huo.
 
Mjadala huo ulikuwa mkali kiasi cha kusababisha watu kumtafuta baba yake mzazi ambaye alikiri kuwa mtoto wake huyo alighushi umri wake kwasababu hakuzaliwa mwaka huo alioutaja kwenye nyaraka zake za kuombea hati ya 
 
Baada ya kuthibitika kwamba umri uliotajwa na Masauni si halisi, Naibu Waziri huyo alianza kuandamwa na hatimaye aliamua kujizulu mbele ya  Baraza Kuu la UVCCM lililoketi mkoani Iringa mapema  2010.
 
Vuguvugu la kumng’oa Masauni lilianza mapema na mpango huo ulisukwa vyema na waliokuwa wakiimezea mate nafasi hiyo hivyo mara tu kikao hicho kilipoanza kwenye ukumbi wa Siasa ni Kilimo, Masauni alianza kushambuliwa kuhusu shutuma zinazomkabali na hatimaye kuamua kubwaba manyanga.
 
Baadhi ya wajumbe walisema hawako tayari kuingia katika kikao hicho kama ajenda ya kumjadili Mwenyekiti Masauni haitakuwepo na ajenda hiyo ilipowasilishwa tu Masauni hakuwa na chaguo zaidi ya kung’oka.
 
Lakini tangu ithibitike kuwa ameghushi umri wake, hakuna hatua zozote za kisheria alizochukuliwa na wala hajawahi kufikishwa mahakamani jambo ambalo lilianza kuzua maswali kama kuna watu wako juu ya sheria.
 
Hatua ya Rais Magufuli kumjumuisha kwenye Baraza la Mawaziri kumeelezwa kwamba ni sawa makosa kwani mtu aliyewahi kuthibitika kuwa ameghushi cheti hawezi kuwa na sifa ya kuteuliwa kuongoza ofisi ya umma.
 
Rais mstaafu Jakaya Kikwete alithibitisha Masauni kudanganya umri akiwa Mwenyekiti wa CCM Mei, 2010.
 
Kikwete alikaririwa akisema Masauni hakuonewa wala kufanyiwa fitina bali alijiuzulu kutokana na kudanganya kuhusu umri wakati wa mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa Jumuiya hiyo 2008.
 
Kikwete alisema kuwa Masauni alitamka kuwa alizaliwa mwaka 1979 wakati uchunguzi ulibaini kuwa alizaliwa Oktoba, 1973.
 
Kikwete aliyasema hayo baada ya kufungua kambi ya wiki moja ya UVCCM kwa ajili ya maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2010 katika Kijiji cha Ihemi, wilayani Iringa Vijijini, Mkoa wa Iringa, ambapo aliongeza kuwa Masauni hakuwa mkweli na kwamba uamuzi wake wa kujiuzulu usingeepukika.
 
Alisema kuwa suala la umri sio tukio la kwanza katika UVCCM kwa kuwa kuna baadhi ya wanachama wake waliozuiwa kugombea nafasi fulani za uongozi kutokana na kuzidi umri.
 
Mwenyekiti huyo wa CCM alisema: ”Hakuna uchawi, ni kanuni na ni lazima kusimamia sheria na kanuni, hatutafumba macho.” 
Kabla ya uchaguzi wa UVCCM 2008 kulitokea mvutano wa makundi yaliyokuwa yanataka kusimika watu wao kwenye nafasi ya Mwenyekiti, hasa kutoka Bara. 
 
Mvutano huo ndio ulimlazimu Mwenyekiti wa Chama,  Kikwete wakati ule kuamua kiongozi wa UVCCM apatikane kutoka Zanzibar ili kutuliza hali ile ya makundi, hali iliyomuibua Masauni kuwa Mwenyekiti.
 
Gazeti hili lilifanya jitihada za kuzungumza na Masauni mwenyewe na mkuu wake wa karibu, Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga, lakini jitihada hizo hazikuzaa matunda baada ya simu zao kuita muda mwingi bila kupokelewa.
 
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa naye alipotafutwa atoe ufafanuzi wa madai ya watu kwamba Rais Magufuli amemteua mtu mwenye kashfa,  simu yake ya mkononi iliita muda mrefu bila kupokelewa jana Jumamosi.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment