dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, April 6, 2016

Waziri wa Magufuli alimpua JK mbele ya Kamati ya Bunge

NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla, amesema Serikali ya Awamu ya Nne chini ya Rais mstaafu, Jakaya Kikwete, inapaswa kulaumiwa kutokana na uzembe uliosababisha kudodora kwa huduma katika Taasisi ya Kansa ya Ocean Road jijini Dar es Salaam.





Dk. Kigwangalla aliyasema hayo wakati uongozi wa taasisi hiyo ukitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa mwaka 2015/16 kwa Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii iliyotembelea taasisi hiyo jana.

“Changamoto kubwa ya hapa Ocean Road ni uzembe uliofanywa na Serikali iliyopita,” Dk. Kigwangalla alisisitiza na kuongeza:

“Kuna taasisi ya kimataifa ilijitokeza kusaidia kununua mashine moja ya mionzi na iliahidi kutoa nusu ya gharama (Sh. bilioni nne), lakini kukawa na uzembe. Tumeanza kufuatilia, tumeomba Hazina watupatie fedha tununue walau mashine moja maana hizi mbili zilizopo zimeshazidiwa.”Aidha, Dk. Kigwangwalla alikiri wizara yake kutegemea wahisani kujiendesha kutokana na changamoto kubwa inayowakabili ya ukosefu wa fedha.”

“Sisi kwenye wizara, tunategemea misaada ya nje kwa asilimia 60, ndiyo maana muda mwingi tunautumia kukutana na mabalozi na wawakilishi wa taasisi za nje kuwaomba kusaidia huduma za afya nchini,” alisema Dk. Kigwangwalla ambaye pia ni Mbunge wa Nzega Vijijini (CCM).

Awali, uongozi wa Ocean Road ulieleza kushindwa kutekeleza baadhi ya majukumu yake kutokana na ufinyu wa bajeti na kadhia ya serikali kutopeleka fedha za miradi ya maendeleo.

Wajumbe wengi wa kamati hiyo waliopata fursa ya kuchangia taarifa hiyo, walimuomba Rais Dk. John Magufuli, kuitembelea taasisi hiyo.

Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi 'Sugu', alisema: "Udaktari ni wito, lakini udaktari wa kansa ni wito mtakatifu. Nafikiri Rais (Magufuli) anayependa kutembelea Muhimbili, aje hapa (Ocean Road) ale na wagonjwa na naamini baada ya kuiona hali ya hapa inayotisha, pesa za Muungano alizozielekeza kwenye barabara, atazileta hapa."

Mbunge wa Bunda (CCM), Boniface Mwita, alisema upo umuhimu kwa serikali kutenga fedha nyingi kwenye sekta ya afya kuokoa maisha ya wananchi.

"Inasikitisha kuona wafadhili wanajitokeza kusaidia kununua mashine halafu kunakuwa na uzembe serikalini," alisema Mwita na kuongeza:

"Hali ya hapa (Ocean Road) inatisha. Kila kitu kimechakaa.
Badala ya kupeleka fedha za sherehe za Muungano kwenye barabara ya Mwanza, nashauri zitumike kununua mashine za mionzi hapa kuokoa maisha ya watu."

/NIPASHE.

No comments :

Post a Comment