Top Leaderboard Advert

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Zanzibar Diaspora

High class shops @ Fuoni

High class shops @ Fuoni

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Adsense Marquee

Saturday, April 9, 2016

Wengi kusombwa maji mishahara hewa 2016


  • MUDA si mrefu wezi watakuwa wamejulikana na sheria itachukua mkondo wake, wapo watakaosimamishwa kazi, wengine watafukuzwa kabisa... Sakata la mishahara ya watumishi hewa limechukua sura mpya baada ya serikali kuanza uchunguzi kuwabaini watumishi wote waliokuwa wakijilipa mishahara hiyo ili hatimaye wachukuliwe hatua.


Hivi karibuni, Rais John Magufuli alisema kuna mfanyakazi wa Mamlaka ya Mapato (TRA) ambaye anajilipa mishahara 17 ya wafanyakazi hewa.

Kwa mujibu wa Waziri wa Utumishi, Angela Kairuki, watumishi hewa wameshaisababishia serikali hasara Sh. bilioni 7.6 kuanzia Januari hadi Machi.

Habari za uhakika kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), zilieleza Nipashe kuwa tayari serikali imeanza uchunguzi wake kuwabaini maofisa utumishi waliokuwa wakitafuna fedha hizo ili wakamatwe.

Mtoa taarifa wetu alisema ukamataji huo utahusisha hazina, waliolipa, wafanyakazi wa wizarani na hata Halmashauri, na kwamba ni suala ambalo linahitaji upelelezi wa kitaalamu kuwabaini wahusika.

"Wale waliokuwa wakitajirika na mishahara hewa siku zao zinahesabika na uchunguzi unaofanyika si wa kawaida," kilisema chanzo chetu ambacho hakikupenda kutajwa jina.

"Muda si mrefu watakuwa wamejulikana na sheria itachukua mkondo wake, wapo watakaosimamishwa kazi, wengine watafukuzwa kabisa.

“Inasubiriwa ripoti ya nchi nzima, kwa sasa kazi ya uchunguzi iko katika hatua nzuri sana wale wote waliojilipa hizo fedha watajulikana na hawatakwepa maana ushahidi na vielelezo vya kuwatia hatiani vipo.”

Waziri Kairuki alipohojiwa kuhusiana na watumishi wake kuhusika katika ulipaji mishahara, alisema ni mapema kulizungumzia suala hilo.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene, alisema watumishi ambao watabainika kuhusika kujilipa mishahara ya watumishi hewa watachukuliwa hatua kali.

Akizungumza na waandishi wa habari wiki hii Waziri Kairuki alisema wamebainika wafanyakazi hewa 7,795 kuanzia
Januari hadi Aprili mwaka huu ambao walishalipwa Sh. bilioni 7.6 tangu waache kuwa watumishi wa umma.

Alifafanua kuhusu watumishi hao kuwa kati ya watumishi hewa 4,317, walibainika ndani ya mwezi mmoja, watumishi 3,033 waligundulika mara tu baada ya Rais John Magufuli kutoa tamko Machi 15 kuhusiana na watumishi hewa.

Alisema baadhi ya watumishi hao walishafariki, wengine walishastaafu na wengine ni majina bandia yaliyongizwa na wajanja ili wawe wanachukua mishahara yao.

Alisema kutokana na hali hiyo, ofisi yake imeagiza maofisa tawala wote wa idara za serikali kufanya uhakiki na kujua huyo mtumishi hewa kituo chake cha kazi kilikuwa kipi, kazi alizokuwa anafanya, tarehe ya kuajiriwa, kufa au kustaafu ama kufukuzwa kazi.


/Nipashe

No comments :

Post a Comment