Top Leaderboard Advert

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Zanzibar Diaspora

High class shops @ Fuoni

High class shops @ Fuoni

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Adsense Marquee

Monday, September 26, 2016

Jamaa amsikia kuku akiwika tumboni baada ya kuiba!

Mike Wanjala alipelekwa kwa mganga baada ya jogoo kuwika kutoka 
tumboni mwake. Picha: TUKO

Jamaa mmoja kutoka kaunti ya Bungoma huko Kenya amewashangaza wengi baada ya kudai kumsikia kuku akiwika tumboni mwake muda mfupi baada ya kusemekana kuwaiba kuku wanane.

Siku tatu baada ya kuwaiba kuku wanane, Mike Wanjala alisemekana kuanza kusikia maumivu na sauti ya jogoo kutoka tumboni mwake.


Wanjala alipata nafuu baada ya mamake kulipa pesa nyingi ili aweze kutibiwa na mganga baada ya jogoo kuwika kutoka tumboni mwake. Picha: TUKO

‘Nilianza kuhisi maumivu tumboni kabla ya kusikia jogoo akiwika kutoka tumboni mwangu kisha nikapelekwa kwa mganga kwa matibabu.’ Wanjala alielezea.

Haya yanajiri baada ya jirani yake kutafuta usaidizi kutoka kwa mganga anayejulikana kama ‘Mama Noor’

Baada ya kutibiwa, Wanjala alionywa na wakazi wa eneo hilo dhidi ya tabia yake ya wizi huku mamake akimshukuru mganga huyo kwa kumtibu mwanawe.

No comments :

Post a Comment