dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, September 2, 2016

Kukatwa Mikarafuu Pemba!


  • Wakulima wapoteza shilingi 100.29 milion kwa msimu
Na Haji Nassor, Pemba

WAMILIKI wa mashamba ya mikarafuu kisiwani Pemba, wamepata hasara ya zaidi ya shilingi milioni 100.29 (milioni mia moja na ishirini na tisa elfu), kufuatia mikarafu yao 430 yenye uwezo wa kuzalisha wastani wa pishi 10,750 kavu kwa msimu mmoja, kukatwa na watu wasiofahamika, kuanzia kipindi cha Januari hadi mwezi Juni mwaka huu.

Mikarafuu hiyo yenye umri usiofanana, imeshambuliwa kwa kukakatwa katwa kwa mapanga, kung’olewa na mengine kuchomwa moto, kwa madai ya siuntafahamu ya kisiasa iliopo kisiwani Pemba.

Uchunguuzi umebaini kuwa, mikarafuu hiyo 430 kama ingekuwa hai, inauwezo wa kuzalisha pishi 21,500 kwa kila msimu ambao ni wastani wa pishi 50 kwa kila mkarafuu mmoja kutegemeana na uwezo wa mkarafuu husika.

Kwa bei ya shirika la Taifa la Biashara Zanzibar ZSTC, karafuu pishi moja kavu ambao ni wastani wa kilo moja au kilo moja na nusu, huuzwa kwa baina ya shilingi 12,000 hadi shilingi 14,000 hivyo wakulima hao, wamepoteza kilo 16,125 sawa na wastani wa pishi 10,750 za karafuu kavu kwa msimo mmoja pekee.Aidha uchunguuzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi umebaini kuwa, Mkoa wa kaskazini Pemba hasa wilaya ya Wete ndiko kulikopotea mikarafuu mengin zaidi na kufikia 233, wakati Mkoa wa kusini wilaya ya Chakechake ikikatwa na kuharibiwa mikarafuu 197 yenye umri tofauti.

Aliepoteza mikarafuu mengi zaidi kwa Mkoa wa kusini Pemba ni waziri asiekuwa na wizara maalumu Mhe: Said Soud Said aliekatiwa mikarafuu 166, ikiwemo michanga na iliozaa msimu mmoja akifuatiwa na sheha wa shehia ya Kendwa Sabiha Mohamed Ali mikarafuu 22.

Kwa Mkoa wa kaskazini Pemba, kati ya mikarafuu 233 iliohujumiwa, 151 ni mali ya serikali iliochanganyika na ya mtu binafsi, wakati wananchi wa Kinyasini Azan Mohamed Nassor na Hamad Azan Hamad walihujumiwa mikarafuu 45.



Aidha mwananchi wa shehia ya Mtambwe kaskazini Bakari Mwitani Sheha na Massoud Ali Hamad wa Kiungoni zote wilaya ya Wete, nao walipoteza mikarafuu yake 16 kila mmoja kwa kuatwa katwa kwa mapanga.

Kufuatia matukio hayo, Jeshi la Polisi mkoa wa kusini Pemba, limeshwafikisha mahakamani watuhumiwa 26 wakikabiliwa na tuhuma za makosa mbali mbali, yakiwemo ya ukataji na ung’oaji wa mikarafuu.

Katika kesi hiyo ya jinai no 69, ya mwaka huu, awali watuhumiwa hao walisota rumande kwa muda wa wiki tatu, kabla ya Julai 12 kupanda tena kizimbani na kupatiwa dhamana na mahakama ya wilaya siku hiyo.

Watuhumiwa hao ni pamoja na majina na umri wao kwenye mabano ni Khamis Abdalla Khamis (30), Ame Makame Ame (40), Omar Abdalla Said (30), Alawi Saidi Alawi (40), Mbarouk Rashid Ali (36), Salehe Seif Abdalla (65), Suleiman Hamad Juma (44), Salim Nassor Khamis (74).

Wengine ni Arif Said Hamid (18), Kombo Bakari Kombo (38), Hamad Abrahman Suleiman (52), Mkubwa Abdalla Bakari (69), Hamad Omar Hamad (58), Mussa Juma Omar (38), Mohamed Makame Ali (36), Rashid Ahmed Rashid (28), Ali Abeid Othaman (60) na Masoud Seif Masoud (50) wote wakaazi wa Ziwani Wilaya ya Chake Chake.

Watuhumiwa wengine ni Saleh Said Maalim (30), Ali Assa Ali (34), Adam Ali Rashid (45), Idrisa Said Maalim (40), Mohamed Haji Moahmed (31), Mohamed Abeid Khamis (30), Khalifa Hamdan Maalim (45) na Saleh Abrahaman Juma (54).

Wakizungumza katika matukio hayo baada ya kuhujumiwa mikarafuu yao sheha wa shehia ya Kendwa Sabiha Mohamed Ali alisema kutokana na tukio amerejeshwa nyuma kimaendeleo.

“Mikarafuu yengu karibu tisa ndio imeanza kuzaa msimu huu, kisha wanaikata hapa wamenirejesha nyuma maana kama ingezaa, basi mimi ningepata pato kubwa’’,alifafanua.

Waziri asiekuwa na wizara maalum Mhe: Said Soud Said aliliomba Jeshi la Polisi kufnya kila njia kuhakikisha wahusika walioharibu mali yake wanakamatwa.

“Hujuma hii haielekei kuwa ni sasa, maana ulimwenguni kote siasa huwa kwenye majukwaa au siku ya kupiga kura na sio kwenye kuhujumu uchumi’’,alisema.

Hata hivyo Azan Mohamed Nassor, alilaani tendo la kuihujumu kwa kukatwa mikarafuu yake, jambo lilimshangaaza na kwamba ni la kupangwa.

Awali tokea mwezi Januari mwaka huu, kisiwani Pemba kulikuwa kukiripotiwa mtendo ya kihalifu ya kuhujumu miti aina ya mikarafuu, migomba, nyumb kutiwa moto ambapo kwa sasa hali hiyo imeripotiwa kutuwa kidogo ndani ya mwezi huu.


/ZanziNews.

No comments :

Post a Comment