Top Leaderboard Advert

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Zanzibar Diaspora

High class shops @ Fuoni

High class shops @ Fuoni

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Adsense Marquee

Thursday, September 8, 2016

SAKAYA: adai ‘kuchuniwa’ na wenzake Dodoma!

Mbunge wa Kaliua (CUF), Magdalena Sakaya.

By Waandishi wa Mwananchi
Thursday, September 8, 2016


Mbunge wa Kaliua (CUF), Magdalena Sakaya amesema baada ya kutokea msukosuko ndani ya chama chake na yeye kutangazwa amesimamishwa uanachama, wabunge wenzake hawampi ushirikiano.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na waandishi wa gazeti la mwananchi, Sakaya ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa CUF Bara alielezea jinsi hatua ya kusimamishwa kwake ilivyofikiwa na anavyotengwa.

Sakaya amesema tangu bunge hilo lianze vikao vyake siku ya Jumanne, wabunge wenzake wa CUF wamekuwa hawampi ushirikiano. Amesema hapati ushirikiano wowote na kwamba wamemuacha afanye mambo yake mwenyewe.

“Siwezi kusema kuna ushirikiano, mimi najua ukweli uko wapi, najua kila kitu, yanayosemwa mitandaoni siyo kweli, mimi najua ukweli.”“Yapo mambo mazito yaliyosababisha mpaka Profesa afike mahali pale, hata ningekuwa mimi ningechukua uamuzi ule,” amesema Sakaya.

Akizungumzia mkutano wa Baraza Kuu la Uongozi ulioketi Zanzibar na kumsimamisha uanachama na wenzake 10 akiwamo Profesa Lipumba, Sakaya alisema hakuwa na taarifa ya kikao hicho.

Amesema siku moja baada ya mkutano mkuu wa chama hicho kuvunjika alipokea ujumbe mfupi wa maneno kupitia simu yake ya mkononi ukimjulisha kuhudhuria kikao cha baraza kuu, uliotumwa na kijana ambaye ni muhudumu katika Ofisi za Makao Makuu ya CUF.

“Ujumbe uliingia Agosti 26 usiku ukisema kuwa: ‘Nimejulishwa nikutaarifu kuhudhuria kikao cha Kamati ya Utendaji na Baraza kitakachofanyika Agosti 28 hivyo unatakiwa kushiriki,” alieleza Sakaya.

Kwa mujibu wa Sakaya, kwa kawaida vikao vya ndani wanakubaliana na Katibu wa chama hivyo yeye (Naibu Katibu) ndiye mwenye jukumu la kuandaa ajenda na kuwajulisha wajumbe wa chini yake.

Hata hivyo, Sakaya alisema awali alianza kuhisi kama kuna tatizo baada ya kupata taarifa kuwa mara tu baada ya mkutano mkuu kulikuwa na vikao vya siri vilivyokuwa vikifanyika bila yeye kujua.

“Nilianza kuhisi kuna kitu, nakumbuka Agosti 22 nilikwenda ofisini kama kawaida baada ya ule mkutano mkuu nikaanza kuongea na viongozi kutoka maeneo mbalimbali kwa makundi ili kujua matatizo katika maeneo yao.”

Aliogeza: “Ilipofika saa 6:00 usiku mlinzi alinifuata na kuniambia mheshimiwa tumeambiwa tufunge ofisi hali ya usalama siyo nzuri.”

“Nikajiuliza kuna nini?. lakini sikupinga taarifa hiyo kwa kuhofia kudhurika…Nikawaambia waliokuwapo pale kuwa nimeitwa kikaoni na nikaondoka.”

“Nilipofika nje ya geti nilikuta waandishi, wakanihoji, nilipomaliza kuwajibu maswali yao nikaondoka. Wakati huo huo nikaambiwa kuna kikao kinafanyika Ubungo nikashangaa, kumbe kuna vikao vinafanyika wakati mimi sijui chochote,” alisema Sakaya.

Sakaya alisema Agosti 23 alikwenda ofisini lakini alipofika mkuu wa Ulinzi na Usalama wa chama alimfuata na kumwambia amepewa maelekezo ya kufunga ofisi zote za chama, na kwamba watu wote waondoke na magari yote yaondolewe katika eneo hilo.

“Nikaanza kuhisi kuna kitu kinaendelea. Nikaondoka ofisini, nikampigia simu kwa Naibu Mkurugenzi wa Uchaguzi, Shaweji Mketo na kumwambia nasafiri kuelekea Dodoma kuhudhuria kamati za bunge lakini nashangaa kuna maelekezo nisifunguliwe ofisi,” alisema Sakaya.

No comments :

Post a Comment