Top Leaderboard Advert

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Zanzibar Diaspora

High class shops @ Fuoni

High class shops @ Fuoni

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Adsense Marquee

Thursday, September 8, 2016

TAARIFA KUHUSU MAHUJAJI WA TANZANIA!

Image result for mecca hajj
Mahujaji wa kutoka Tanzania wapatao 2,000 waliwasili salama katika miji mitakatifu ya Makkah na Madina mwishoni mwa mwezi Agosti mwaka huu na tayari wameshaanza kufanya ibada pamoja na ziara hadi katikati ya mwezi Septemba mwaka huu.

Hakuna taarifa zozote za matatizo kuhusu mahujaji wa Tanzania katika maeneo waliyofikia, wote wako salama na afya njema.

Mwaka huu Serikali ya Saudi Arabia imeimarisha miundo mbinu, usafiri, ulinzi, usalama na uangalizi makini kuhakikisha kuwa hakuna dosari zozote zinazoweza kutokea kutokana na uwepo wa wingi wa mahujaji kutoka nchi mbalimbali duniani. 

Takriban mahujaji milioni 2 kutoka mabara yote duniani wapo nchini Saudi Arabia kutekeleza nguzo mojawapo kati ya nguzo 5 za dini ya kiislamu.

Taarifa imetolewa na:
Balozi Hemedi Iddi Mgaza
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia


No comments :

Post a Comment