dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, October 15, 2016

Kenya yasema kujiweka kando kwa Tanzania hakutasababisha nchi zilizokubali kushindwa!

Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania imekataa kuridhia mpango wa matumizi ya visa ya pamoja, ambao umeanza kutekelezwa na nchi za Uganda, Kenya na Rwanda.

Sababu ya kuukataa ni kutoridhishwa na masuala mbalimbali likiwamo la usalama hasa tishio la ugaidi kwenye baadhi ya nchi za Afrika Mashariki.

Mpango huo wenye lengo kuvutia watalii wa kigeni unatekelezwa chini ya mwavuli wa umoja wa hiari na tayari visa 4,000 zimetolewa kwa watalii hao.

Kaimu Mkurugenzi wa Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji wa Mambo ya Nje, Bernard Haule  alisema Serikali haijaridhika na taratibu zizotumiwa na nchi zilizosaini mpango huo nje ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).“Wazo la kuja na visa ya pamoja lilitolewa na Sekretarieti ya EAC,  walilifanyia utafiti ili kubaini changamoto zinazoweza kujitokeza,” alisema.

Kutojiunga kwa Tanzania kwenye mpango huo kunafanya ishindwe kushiriki  kongamano la utalii lililopangwa kufanyika Novemba 7 jijini London, Uingereza baada ya kuandaliwa na nchi hizo tatu.

“Kila nchi itatakiwa kuwa na maofisa wake wa uhamiaji kwenye balozi za nchi wanachama, Tanzania itajiunga pindi mapendekezo yaliyotolewa na sekretarieti yatakapotekelezwa na Serikali kujiridhisha,” alisema. 

Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa  Jumanne Maghembe amesema Tanzania inaendelea kujitegemea katika visa za utalii, kwa kuwa bado haijajiunga na utaratibu huo.

Kuhusu hatua ya kutoridhia mpango huo, Waziri wa Utalii wa Kenya, Najib Balala alisema Tanzania ina wasiwasi wa ushindani kutoka Kenya.

 Alisema nchi hizo zimedhamiria kushirikiana katika sekta ya utalii kwa kuainisha mikakati ya pamoja itakayokuwa chachu ya kuwavutia watalii wa kigeni.  

Balala alisema kujiweka kando kwa Tanzania hakutafanya nchi hizo zishindwe kusonga mbele.

Kupitia ushirikiano huo, watalii watakaoingia katika nchi hizo watalipa ada moja itakayowawezesha kutembelea maeneo yote.

No comments :

Post a Comment