dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, October 22, 2016

KIJIJI CHA MATEMWE (ZANZIBAR) IN 2025!

Mradi Mkubwa wa Ujenzi wa Hoteli ya Kitalii katika Kijiji cha Matemwe Zanzibar Inayojengwa na Pennyroyal (Gibraltar) Ltd Zanzibar.

Mmiliki wa Mradi wa Hoteli ya Kitalii katika eneo la Matemwe Mkoa wa Kaskazini Unguja, Mkurugenzi wa Mradi huo Brain Thomson, akitowa maelezo kwa waandishi wa habari walipofika kutembelea mradi huo kujionea maendeleo ya matayarisho yake na kuwaonesha michoro ya picha za majengo ya Mradi huo mkubwa utakaokuwa na uwanja vya ndege. na kutengeneza visiwa kwa ajili ya wageni wanaofika katika Visiwa vya Zanzibar. 
Mmiliki wa Mradi wa Mkubwa wa Hoteli ya Kitalii katika eneo la Matemwe Mkoa wa Kaskazini Unguja Mr. Brian Thomson, akitowa maelezo ya mradi huo kwa kuwaonesha jinsi ya majengo yatakuwa katika eneo hilo na kutoa ajira kwa Wananchi wa Matemwe na vijiji jirani kupitia mradi huo.   
Mmiliki wa Mradi Mkubwa wa Ujenzi wa Hoteli katika eneo la Matemwe Mkoa wa Kaskazini Unguja Mr. Brian Thomson akizungumza na waandishi wa habari walipofika kuangalia ujenzi wa mradi huo na kusema kukamilika kwakev kutachukua miaka minane kukamilika kwake na kutowa fursa za ajira kwa vijana wa kijiji hicho na kutowa maendeleo katika sekta za jamii kunufaika na mradi huo.
Sehemu ya mbele ya majengo ya mradi huo kuingia katika eneo la hoteli hiyo.
Jinsi ya mradi huo utakapokamilika ujenzi wake utakuwa kama hivi na kubadilisha mandhari ya eneo la matemwe mkoa wa kaskazini unguja.















Na Salum Vuai, MAELEZO

JAMII visiwani Zanzibar imeombwa kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wawekezaji wanaoonesha nia ya kuwekeza miradi ya maendeleo yenye mwelekeo wa kubadilisha maisha ya wananchi na kuwatoa kwenye umasikini.


Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya kutembelea eneo la Matemwe ambako kampuni ya Penny Royal inajenga kijiji cha utalii, mwanaharakati Rashid Yussuf Mchenga, amesema Zanzibar haiwezi kujitenga na dunia, hivyo hapana budi kuwapokea kwa mikono miwili wawekezaji wenye nia njema.

Alitaka dhamira ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuwafungulia milango wawekezaji wa nje iungwe mkono na kila mpenda maendeleo, kwani uchumi wa visiwa hivi unahitaji ushirikiano wa kila hali na taasisi zenye mitaji mikubwa ya kuwekeza miradi yao hapa nchini zikiwemo za kigeni.

Mchenga ambae pia ni Katibu Mwenezi Taifa wa chama cha ADA-TADEA, amesema mradi huo utakaokuwa wa aina yake, ni neema ya kushukuriwa na wananchi wa Matemwe, mkoa wote wa Kaskazini na Wazanzibari kwa jumla.

“Kama tunavyosikia kwamba mradi huu utaajiri zaidi ya wananchi 1,500 katika hatua za awali, hii ni fursa muhimu ya kuwasaidia vijana wetu kuondokana na tatizo la ajira,” alifahamisha.

Hata hivyo, alisema kustawi kwa miradi ya maendeleo katika nchi yoyote lazima kuende sambamba na kuimarika kwa hali ya amani na usalama, kwani bila vitu hivyo, hakuna jambo la maendeleo linaloweza kufanyika.

Meneja wa Penny Royal Brian Thompson, amesema miongoni mwa mipango yao katika kuufanikisha mradi huo, ni kushirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, kuandaa utaratibu wa mafunzo ya lugha ya Kiingereza kwa vijana, pamoja na elimu ya kazi zinazohusiana na utalii ili kuwaandaa kwa ajili ya ajira zitakazopatikana.

Alisema ujenzi wa kijiji hicho utakaogharimu zaidi ya dola bilioni moja, unatarajiwa kukamilika kabisa baada ya miaka minane, ukifanyika kwa awamu mbili, ambapo kila moja itachukua miaka mine.

Mradi huo mkubwa na wa kwanza wa aina yake hapa nchini, utajumuisha ujenzi wa skuli, hospitali, kituo cha polisi, kituo cha jamii kwa wajasiriamali, uwanja wa ndege, kiwanja cha Golf na ujenzi wa visiwa vidogo vidogo pamoja na mkahawa maalum utakaojengwa chini ya bahari.

No comments :

Post a Comment