dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, October 23, 2016

Madiwani CUF Watwangana Ngumi Hadharani!


Polisi mjini Tanga jana walilazimika kuingilia na kuzima vurugu zilizotokea katika ofisi za Chama cha Wananchi (CUF), Wilaya ya Tanga zilizotokana na madiwani kugawanyika katika makundi mawili. 

Makundi hayo ya madiwani yaligawanyika kuhusu uamuzi wa wenzao waliohudhuria kikao cha baraza la madiwani wa jiji hilo Oktoba 12.

Vurugu zilianza baada ya Mwenyekiti wa CUF wilayani humo, Rashid Jumbe ambaye pia ni diwani wa Mwanzage aliyegombea nafasi ya umeya kuamuru madiwani waliohudhuria baraza hilo watoke nje ili wajumbe waanze kumjadili mmoja mmoja.

Baada ya amri hiyo kundi la madiwani 12 waliotolewa nje kusubiri kuhojiwa waliamua kuingia kwa nguvu kutaka kumtoa Jumbe wakidai anasababisha makundi ndani ya chama hicho. Vurugu ziliendelea kwenye mlango wa kuingilia, jambo lililosababisha wanachama waliokuwa nje kuingilia kati, huku wakirushiana ngumi.

Baadaye magari matatu ya polisi yaliwasili katika ofisi hizo na kuwatawanya wanachama waliokuwa wamejaa, jambo lililomsaidia Jumbe kufanikiwa kutoka.

 Akizungumza baada ya vurugu hizo, Jumbe alisema kikao hicho kilikuwa na ajenda ya kuwahoji na kisha kuwajadili madiwani waliohudhuria baraza hilo kinyume na msimamo wa CUF.

Katibu wa CUF wa wilaya hiyo, Thobias Haule ambaye pia ni diwani wa Mnyanjani alisema madiwani waliohudhuria kikao cha baraza hawakwenda kinyume na chama kwa sababu waliamua kuwawakilisha wananchi waliowachagua, badala ya kuendeleza mgomo ambao hauwasaidii.

“Tukubali kwamba kwa kipindi cha mwaka mmoja tulichokaa bila kushiriki vikao vya baraza kuna mambo mengi ya maendeleo ya wananchi ambayo hayakufanyika, tumeamua kuhudhuria kwa masilahi mapana ya wananchi,”alisema Haule.

Mbunge wa Tanga Mjini, Mussa Mbarouk aliwataka wanachama wao kuwa wavumilivu kwa viongozi wako imara na hawatakubali kuyumbishwa.

 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba alisema Jumbe alifikishwa Kituo cha Polisi Chumbageni kuhojiwa kuhusu sakata hilo. Halmashauri ya Jiji la Tanga ina jumla ya madiwani 36; CUF inao 20 na CCM wako 16.

No comments :

Post a Comment