dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, October 26, 2016

Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Balozi Amina Salum Ali Azindua Baraza Jipya la Kusimamia Mfumo wa Utoaji wa Leseni!

Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Balozi Amina Salum Ali akizindua Baraza jipya la Kusimamia Mfumo wa utoaji leseni Ofisini kwake Migombani, Mjini Zanzibar.

Katibu Mtendaji wa BLRC Rashid Ali akitoa maelezo mafupi ya shughuli za Baraza hilo wakati wa uzinduzi rasmi uliofanywa na Waziri Amina Salum Ali Ofisini kwake Migombani.

Mwenyekiti wa BLRC Vuai Mussa Vuai akitoa shukrani zake kwa niaba ya wajumbe wa Baraza hilo baada ya kuzinduliwa rasmi na Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Amina Salum Ali.
Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Zanzibar Mhe Balozi Amina Salum Ali akiwa katika picha ya pamoja ya Wajumbe wa Baraza la Kusimamia Mfumo wa Utoaji Leseni Zanzibar, baada uzinduzi wa Baraza hilo.migombani.(Picha na Ramadhani Ali)

Na. Ramadhani Ali/Maelezo Zanzibar.
Baraza jipya la Kusimamia Mfumo wa Utoaji Leseni (BLRC) limeagizwa kusimamia mfumo huo kwa mujibu wa sheria ya mwaka 2013 ili kuondosha kasoro zilizojitokeza katika mfumo wa zamani na kurahisisha ufannyaji wa biashara Zanzibar.

Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko Balozi Amina Salum Ali ametoa maagizo hayo Ofisini kwake Migombani alipokuwa akizindua Baraza hilo lenye wajumbe 13 kutoka Taasisi za Serikali na watu binafsi likiongozwa na Mwenyekiti wake Vuai Mussa Vuai.

Amesema mfumo uliokuwa ukitumika wa utoaji leseni za biashara ulikuwa sio rafiki kwa wadau, ni wenye unaurasimu na  unachukua muda na pia unagharama  kubwa katika upatikanaji wa baadhi ya leseni.

Ametaja  kasoro nyengine za mfumo wa zamani wa utoaji leseni  kuwa ni kuwepo kwa sheria na vyombo vingi vya utaji leseni, kutokuwepo msimamizi wa vyombo hivyo na kuwepo kwa aina tofauti za leseni, vibali au ruhusa ya kuendesha biashara ambazo zote zina lengo moja.

Balozi Amina amelitaka Baraza hilo katika kutekeleza majukumu yake kuondosha urasimu na kupunguza muda katika utaratibu wa kuomba na utoaji leseni, kusimamia utaratibu rahisi na wa kupunguza gharama katika upatikanaji wa leseni na kuwepo masharti ya kusimamia biashara.

Aidha amelielekeza Baraza kuzingatia misingi na vigenzo katika utoaji wa leseni, kusimamia uanzishaji wa mfumo wa kielektroniki katika utoaji wa leseni kwa mamlaka zinazotoa leseni na kuhakikisha malipo ya leseni yanalipwa kupitia benki kila inavyowezekana.

Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko amelishauri Baraza kuanzishwa daftari maalum la leseni, vibali na ruhusa nyengine katika katika kuendesha biashara na kupendekeza mfumo bora wa utoaji leseni za biashara kwa kuzingatia mazingira ya nchi nyengine zenye kufafana na Zaznzibar.

Amesema Wizara yake imegundua  zipo biashara nyingi zimepewa leseni bila kusajiliwa kwa wakala wa usajili hivyo ametaka kuhakikisha biashara zote
zinasajiliwa kwa wakala wa usajili wa Biashara na Mali kabla ya biashara hizo kupewa leseni.

Mwenyekiti wa Baraza la Kusimamia Mfumo wa utoaji Leseni Vuai Mussa Vuai amemuhakikishia Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko kuwa Baraza hilo litafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa ili kuhakikisha malengo ya kuazishwa kwake yanafikiwa.

Ameahidi kuwa  watafuata sheria na kanuni za mfumo huo mpya wa utoaji wa leseni za biashara ili kupunguza kasoro nyingi zilizojitokeza katika katika mfumo uliokuwa ukitumika kabla.

1 comment :

  1. Thank you for your articles that you have shared with us. Hopefully you can give the article a good benefit to us. Driving Test Cancellations Checker

    ReplyDelete