dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, October 22, 2016

Yaliojiri Katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki. Zanzibar.!

Na Mwashamba Juma.
WAJUMBE wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) wamesema tatizo la fedha linaloikabili Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) sio suala la serikali moja moja bali ni la nchi wanachama wote.

Walisema changamoto hiyo imekuwa sugu na ya muda mrefu, hali waliyoielezea kuchangia kuteteresha uchumi wa jumuiya hiyo na kusababisha kusimama kwa baadihi ya kazi za jumuiya.

Wakijadili hoja ya pamoja kwenye kikao cha tano cha mkutano wa pili wa bunge la tatu la EALA, huko ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani mjini Unguja, hoja iliyowataka wajumbe hao kuwa na njia mbadala ya kuichangia EAC kutokana na uhaba wa fedha unao ikabili jumuiya hiyo.

Wajumbe hao wa bunge la EALA walishauriana kusimama pamoja na kutumia sauti ya moja ili kukabiliana na changamoto zilizopo mbele yao.Akichangia hoja iiliyowasilishwa bungeni hapo kwakuzungumia mbinu mbadala walizojadiliana kutatua changamoto hiyo, Mbunge wa Afrika Mashariki anaeiwakilisha Tanzania kwenye jumuiya hiyo, Mhe. Maryam Ussi Yahya alisema licha ya changamoto za kiuchumi zinazoikabili EAC anaamini bado itaendelea kusongambele katika kuyafikia malengo iliyojiwekea.

Alieleza suluhu ya kuondosha tatizo liliopo sio suala la siku moja bali linahitaji mda hadi hali kutengemaa.

Alisema asilimia kubwa ya mapato ya jumuiya hutegemea ufadhali kutoka Jumuiya za kimataifa, hali iliyochangia kukwamisha kwa baadhi ya shughuli za EAC.

"Si kama tunataka jumuiya iendelee kutegemea wafadhili kutoka nje, tunachotaka nchi wanachama tuchangie asilimia mia moja kwaajili ya kuiinua jumuiya yetu" alieleza Mhe. Yahya.

Alisema wajumbe wanamatumaini makubwa kuwa jumuiya itazidi kusongambele licha ya kukabiliwa na changamoto za fedha zilizosababisha kuzorotesha kwa baadhi ya kazi za jumuiya hiyo.

Nae Mbunge kutoka Jamuhuri ya Kenya, Peter Mathuki alieleza mjadala uliopo mbele yao ni muhimu kwani unajadili hatima ya wanachi wa mataifa matano ya Afrika Mashariki, hivyo azitaka nchi wanachama za EAC kutumia maliasili zao kwa ufanisi sambamba na kutekeleza miradi yao ya maendeleo kwa kuhakikisha inaiongezea mapato jumuiya ili kupunguza tatizo la uhaba wa fedha linaloikabili jumuiya hiyo.

Akizungumzia suala la ushirikiano kwa nchi wanachama wa EAC katika kukabiliana na changamoto ya fedha inayowakabili, Mbunge kutoka Uganda, Dora Byamukama alilisitiza kufanyakazi pamoja kwa sauti moja kwaajili ya kuiendeleza EAC ya sasa na baadae ili isitetereke kwa changamoto za kiuchumi.

Kwa upande wake Martin Ngoga, Mbunge kutoka Rwanda wakati akichangia hoja hiyo bungeni hapo, alieleza wajibu wao kama nchi wanachama kuangalia mbinu mbadala za kudhibiti hali ya fedha ya jumuiya yao isidhorote.

Akizungumzia juhudi za haraka zilizochukuliwa na Jumuiya hiyo ili kuiokoa kutoka kwenye hali mbaya ya mgogoro wa fedha unaoikabili, Katibu mkuu wa Jumuiya hiyo ambae pia ni Mbunge anaeiwakilisha Burundi katika bunge la EALA, Mhe. Libera Mfumukeko alisema EAC imefanikiwa kukusanya kiasi cha dola milioni tano kutoka kwa nchini wanachama wake.

"Wiki mbili zilizopita, Jumuiya yetu ya EAC imepokea dola milioni tano kutoka kwa wanachama wake ikwemo Burundi iliyochangia dola milioni 2. 8" alieleza.

Alizitaja nchi nyengine zilizochangia kiasi hicho cha fedha ni pamoja na Kenya dola milioni mbili na mwenyeji Tanzania dola milioni moja na kuongeza kuwa nchi za Rwanda na Uganda wanategemea kuchangia siku za karibuni.

Mfumukeko ambae pia ni mhasibu mkuu wa EAC alieleza kwasasa hali ya fedha kwa jumuiya hiyo kidogo inaridhisha ambayo inaweza kuisukuma walao kukidhi mahitaji yake ya lazima.

Sambamba na kueleza kuwa EAC bado inapambana kufanikisha juhudi zaidi sio kwa kupata misaada kutoka kwa wafadhili na wadau wa maendeleo pekee, hata kwa juhudi za wakuu wa nchi wanachama wa jumuiya wakiwemo maraisi wa nchi tano zinazounda jumuiya hiyo ya EAC.

Akizungumzia michango ya wadau wao wa maendeleo kwenye jumuiya hiyo, Mfumukeko alieleza awali walichelewa kuchangia ndio maana EAC ilitetereka kifedha nakuongeza kuwa siku chache baada ya kikao hicho cha tano cha bunge la tatu la mkutano wa pili wa EALA kuna baadhi yao walijitokeza kuichangia EAC, wakiwemo Wajurumani, Norway na Denmark.

Pia alieleza kuwa EAC walisaini mkataba wa Euro milioni 85 kutoka kwa Umoja wa Ulaya (EU) na kueleza kiasi hicho cha fedha kitakachoingia kitasukuma miradi mingi ya maendeleo ambauo EAC imejipangia kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.
Aliongeza kuwa EAC pia imesaini na shirika la kimataifa la (US aids) mkataba wa dola milioni 50.

Hata hivyo alieleza uhusiano wa EAC na wadau wake wa maendeleo bado unaendelea vyema licha ya kuwepo kwa baadhi ya changamoto zilizochelesha kuchangiwa fedha mapema miongoni mwao alizieleza ni pamoja na migogro ya ndani ya EU ikiwemo Kujitoa kwa Uingereza na ongezeko la wakimbizi kwenye nchi za Ulaya limeicheleweshea EAC kupokea misaada kutoka kwa jumuiya hiyo.

Mapema akiwasilisha hoja hiyo ya pamoja iliyowataka wajumbe wa bunge la EALA kutafuta mbinu mbadala za kuichangia jumuiya ya EAC kutokana na uhaba wa fedha unaoikabili, Mbunge kutoka Kenya Judith Pareno alieleza migogoro ya fedha inayoikabili EAC imekuwa mikwazo cha kusumuma mbele miradi ya maendeleo na uchumi wa jumuiya hiyo kwa nchi wanachama wake.

Mkutano wa pili wa bunge la tatu la EALA pia uliwasilisha mswada wa " Kudhibiti usafirishwaji wa binaadamu katika nchi za Afrika Mashariki" ambao liwasilishwa na Mhe. Maryam Ussi Yahya, Mbunge wa Afrika Mashariki anaeiwakilisha Tanzania.

Aidha spika wa bunge hilo la EALA, Mhe. Daniel Kidega alikighairisha kikao hicho hadi Oktoba 18 mwaka huu kwaajili ya kuujadili mswada wa " Kudhibiti usafirishwaji wa binaadamu katika nchi za Afrika Mashariki".

No comments :

Post a Comment