dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, November 3, 2016

Lukuvi: Marufuku kwa Diaspora kumiliki ardhi nchini!

Waziri wa Ardhi Mh Wilam Lukuvi

Amesema taarifa hizo zitaisaidia serikali kuzitwaa ardhi hizo kwa kuwa raia wa kigeni hawaruhusiwi kumiliki ardhi nchini na kufanya hivyo ni kukiuka sheria.

Akitoa hotuba kwenye mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wapima Ardhi Tanzania (IST), Mhe. William Lukuvi amesema anayeruhusiwa kumiliki ardhi nchini ni raia wa Tanzania pekee na kuongeza kwamba kwa watanzania waishio nje ya nchi na kuukana uraia wao nao hawataruhusiwa kumiliki ardhi bali watapewa ardhi kama ilivyo kwa wawekezaji kutoka mataifa mengine.

“Mtu akishaukana uraia wa Tanzania hana haki tena kama raia wa Tanzania, hivyo atamiliki ardhi kama mwekezaji na siyo raia, ardhi itabaki kuwa ya Watanzania tu, tutawasaka wale wote ambao wanamiliki ardhi kinyume na sheria za nchi,” amesema Mh. Lukuvi.

Aidha, Mhe Lukuvi amewataka wapima ardhi Tanzania kuhakikisha wanatimiza lengo la serikali la kupika na kutoa hati 400,000 ifikapo mwezi Juni mwaka 2017 pamoja na kutenga maeneo ya wafugaji kila wapimapo ardhi.

Wadau hao wa upimaji ardhi wamesema, watahakikisha wanatimiza lengo la serikali la kupima na kutoa hati 400,000 ifikapo Mwezi Juni2017 kwa kutumia vifaa vya kisasa sambamba na kuwekeza hasa mikoani ili kutoa fursa sawa kwa watanzania kupata hati za ardhi yao.


/ EATV

No comments :

Post a Comment