dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, November 1, 2016

Rais Santos ‘mahakamani’ kwa tuhuma za upendeleo Angola!


LUANDA, ANGOLA

MAHAKAMA ya Juu ya Angola imemuamuru Rais Jose Eduardo dos Santos kujibu tuhuma za kumteua binti yake Isabel kuongoza Kampuni ya Taifa ya Mafuta ya Sonangol.

Dos Santos alimteua binti yake huyo bilionea kuwa mtendaji mkuu wa kampuni hiyo Juni mwaka huu.

Uamuzi huo wa mahakama umetokana na kuanza kuyafanyia kazi maombi ya shauri lililowasilishwa mahakamani hapo na wanasheria 14 wa Angola.

Wanasheria hao wanaomtuhumu kiongozi huyo mkongwe nchini hapa kuendekeza undugu na kuvunja sheria ya uaminifu ya nchi hiyo.

Hata hivyo, si rais mwenyewe, msemaji kutoka kitengo cha mawasiliano cha Ikulu wala Isabel mwenyewe, aliyepatikana mapema wala kupokea simu kuzungumzia mwito huo wa mahakama.

Isabel, ambaye ni bilionea namba moja mwanamke barani Afrika kwa mujibu wa Jarida la Forbes la Marekani, aliteuliwa kuchukua mamlaka hayo mara baada ya hatua ya kushtukiza ya baba yake kuivunja Bodi ya Sonangol.

Miongoni mwa hatua, ambazo Isabel aliahidi kuzichukua dhidi ya kampuni hiyo ni pamoja na kuigawanya katika vitengo vitatu; uzalishaji, usafirishaji na kitengo kitakachohusika na mikataba.

/Mtanzania

No comments :

Post a Comment