dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, March 19, 2017

RC Makonda avamia Clouds na kuwatisha SHILAWADU!




Makonda hua anafika office za clouds mara kwa mara. Siku zingine anashinda hapo mpaka jioni. Siku ya Alhamis Makonda alifika office za Clouds Cha ajabu siku hiyo alikaa mpaka usiku akawa anamtafuta soudy Brown na Qwisser wa SHILAWADU muda huo walikuwa bado hawajafika kazini basi akawa anazungukazunguka tu ofisi hii anatokea ile kama mfanyakazi wa Clouds.

Kwenye Mida ya Saa kumi hivi akakutana na kina Soudy pamoja na prodyuza wa kipindi wakawa wanaongea kwa uficho hivi na usiri tukajua tu ni mambo ya kawaida ya kuhitaji uprivate lakini siku ile ulikuwa unatia mashaka sana.

Kumbe Makonda alikuja na Story ya mwanamke mmoja ambaye yeye Makonda alisema huyo mwanamke amezaa na mchungaji Gwajima na ametelekeza akawa anataka arekodiwe na ubuyu uruke kwenye kipindi cha SHILAWADU.

Basi wakakubalia kwa kuwa ni habari itabidi huyo mwanamke arekodiwe na kipindi kiruke siku ya jana lakini kawaida ya Kipindi cha SHILAWADU ubuyu ukipatikana lazima kila mtu apewe Natural Justice ya kusikilizwa pande zote mbili sababu huwa ndiyo kawaida ya kipindi.


Makonda siku hiyo hiyo ya Alhamisi akamwambia Soudy ajiandae then huyo mwanamke mnayemuona kwenye video na mtoto aliletwa na wasaidizi wa Makonda ahojiwe na Soudy Brown tayari kwa kurushwa kwa kipindi.

Siku ya Ijumaa ambayo ilikuwa ni jana SHILAWADU wakamtafuta Gwajima kwa upande wake kama anaifahamu hiyo ishu na je mwanamke huyo aliyetajwa ni kweli kwasababu tunaelewa ugomvi uliopo kati ya Makonda na Gwajima isijekuwa SHILAWADU wanatumika kuwafitinisha watu vibaya!

kwa bahati mbaya Gwajima hakupatikana jana ijumaa kwa ajili ya kurekodiwa na kufanyiwa mahojiano.

SHILAWADU wakatumia busara mpaka apatikane Gwajima scene ya Dada mwenye mtoto ziende kwa pamoja na ya mchungaji Gwajima kama kawaida ya POVU inavyokuwaga.

Jana usiku sasa kumbe Makonda alikuwa anafuatilia kipindi cha SHILAWADU aone kama kile kipande kitaruka hewani wapi ndiyo akaamua kuja Clouds na magari mawili yeye mwenyewe Makonda na Watu kama nane hivi wakiwa na Bunduki aina ya SMG geti la kawaida mlinzi alifungua geti kwasababu amezoeleka Mh anakujaga mjengoni wakafunguliwa kisha wakaingia ndani.

Walipofika reception wakazuiwa kuingia ndani sababu hatuna utaratibu wa kuruhusu wageni baada ya saa Nne usiku kuingia ndani ya Ofisi kama siyo mfanyakazi wa CLOUDS.

Alipoona wanazuiwa wakatoa bunduki zao mlinzi akashurutishwa afungue mlango kwa nguvu sababu walimtishia na Silaha mlimzi akafungua mlango wakaenda naye hadi studio kipindi kilikuwa kinaendelea hewani.

Makonda akawatoa nje Soudy na Mwenzake Qwisser akawauliza kwanini video aliyowaletea haijachezwa wakaelezea utaratibu jinsi utaratibu ulivyokuwa Qwisser wakati anajielezea akapigwa mtama akaanguka chini wakavamia mitambo ya transmission kwenye traycaster wakitaka kile kipande kirushwe hewani prodyuza wa kipindi akamuambia Makonda kwanini anavunja utaratibu na kutumia nguvu na ameshapewa utaratibu akapigwa na kitako cha Bunduki mgongoni akaanguka chini bahati mbaya kipindi kilikuwa kimefika mwisho.

Wakamshurutisha Prodyuza wa SHILAWADU anaitwa Chriss awape kile kipande wakaondoka naye wakati wanaondoka Ruge alikuja na Polisi akaingia lakini tayari walikuwa wameondoka ofisini wamechukua hicho kipande cha Video ya huyo mwanamke.

Hizo video zilichukuliwa kwa nguvu na Makonda na hao watu waliokuwa na Silaha inasemekana Makonda ana timu yake wanazisambaza kwa kasi na hatujui lengo lake ni nini.

Hata mkihitaji footage za Camera zipo jinsi tukio lilivyokuwa usiku wa jana.


====
Kutoka kwa wadau wa Clouds Media

https://www.jamiiforums.com/threads/rc-makonda-avamia-clouds-na-kuwatisha-shilawadu.1219107/

https://www.jamiiforums.com/threads/mwanamama-kupitia-uhuru-fm-adai-kuzalishwa-na-askofu-gwajima-na-kutelekezwa.1218958/

3 comments :

  1. Aaah! Kweli siku ya kufa nyani majani yote huteleza. Why do that?

    ReplyDelete
  2. Km hayo ni kweli basi Makonda ni mshirika wenu nyie clouds.. Cha kufanya ni kutafuta msuluhishi,.. Na ku-redefine mahusiano yenu na mkubwa huyu mliyempenda... Kwani huyu mkubwa si anajua kila kitu ndani ya studio ZENU? Ametumia mabavu (kama ni kweli) akachukua CD yake yenye clip ya huyo mzinifu (km ni kweli)... Mimi nafikiri Mh. Makonda hana haja ya kujibizana na RAIA mdogo km Gwajima.. Km ni kweli kuna forgery ya vyeti uzinifu wa askofu sio utetezi... Askofu sio mwajiriwa wa SERIKALI kwa hiyo hayo ni mambo binafsi.... NARUDIA, WATU WENGI WAMEPITIA HATUA NYINGI HADI KUPATA ELIMU WALIYO NAYO... WENGI SANA WANATUMIA MAJINA AMBAYO SIYO YAO... WALIJIENDELEZA KWA MAJINA YA WATU WENGINE.... UTARATIBU HUO UPO HADI LEO... MTOTO AKIFELI KIDATO CHA 4 ANARUDIA K.3 AU CHA 4 KWA JINA LA MWENZAKE ALIYEACHA SHULE... NI KAWAIDA TU........ PILI, KAZI YA UKUU WA MKOA SIYO YA KITAALAM... NI YA KUSIMAMIA MAENDELEO KWA UJUMLA NA PIA ULINZI NA USALAMA... KTK HILI CHETI SIYO ISSUE !!

    ReplyDelete
  3. Eh Twaha,
    Are u crazy my friend? Cheti sio issue kwenye hili kakuambia nani? Wapi tena cheti kitakuwa ni issue. Cheti kina issue in every respect of your life. Kama umeweza kudanganya huko nyuma basi ujue utadanganya tena na tena na tena kwa mambo mengine. Umeona alivyojilimbikizia magari ya watu? Hivyo ni akili ya mtu hii?
    Magufuli anajiharibia kumuachia huyu kijana mpaka leo. Mwisho kila mtu DSM atamgomea - wakati huo atafanya nini? Hii inaonesha kuwa mkuu wetu pia ni mkaidi. This guy is no good. He should have fired him on the first day na yote haya yasingelijitokeza. Sasa tizama hayo mambo yanayofichuka ambayo tusingeliyajua kama angelitumbuliwa zamani. Sasa Magufuli anaji-embarrass mwenyewe kwa kila anavyomuachia zaidi kukaa kwenye position ya RC. Huyo mtoto will never be rejuvenated. Amekwisha kifikra na kimawazo.
    Hivyo mtu mwenye akili yake timamu angeliingia kwenye Clouds TV kama vile? Inaonesha hana akili na ndio maana alipata masufuri tu shuleni!
    Huyu tena ni mtoto hatari sana. Bora alivyojulikana mapema. Angelituletea mabalaa zaidi huko mbele kama angepanda juu zaidi. Mungu amemfichua hadharani na hakuna anaemtaka hivi sasa labda mzee Magufuli peke yake. Kwa aibu yote hii anayoitia serikali bado amemkumbatia tu!!! Ni ajabu sana. Now we see the other side of the bull-dozer, kumbe sio kusukuma tu bali nakuchimba pia!

    ReplyDelete