dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, June 25, 2017

health: Faida 10 za kunywa maji ya limao kila siku asubuhi

Pindi utakapoamua kunywa maji ya limao kwa kila siku asubuhi unaweza ukapata faida zifuatazo;

1.Huongeza Kinga yako ya mwili hasa kupambana na magonjwa madogo kama mafua, na kikohozi kutokana na kuwa na vitamin C

2. Husafisha Mfumo wako wa chakula, kuondoa sumu mwilini na kuzuia tumbo kujaa gesi mara kwa mara

3. Huleta hewa safi kinywani. Ni Muhimu sana kwa watu wanaonuka midomo

4. Hukuongezea uchangamfu na kufanya siku yako ianze vizuri sana5. Husaidia majeraha kupona kwa haraka kutokana na kuwa na ascorbic acid ya kutosha. Pia huimarisha mifupa

6. Husaidia mmeng’enyo wa chakula utakachokula asubuhi au mchana kwa kuondoa vikwazo vyote vinavyoweza kuzuia umeng’enyaji wa chakula.

7. Himarisha Ngozi yako, kuondoa makunyanzi na kukupa muonekano mzuri.

8. Husaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza uzito kwani maji moto ya limao huyeyusha mafuta ya kutosha.

9. Huyapa macho yako afya nzuri na kuimarisha kuona.

10. Huondoa hali ya kuhitaji kahawa kila asubuhi ambayo si nzuri kiafya.

Muhimu; kamua maji ya limau na unjwe walau mara mbili kwa siku kwa muda wiki moja mfululizo utaona matokeo yake.

No comments :

Post a Comment