dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, June 28, 2017

Mwanza: Mtoto wa miaka mitano abakwa!

Mtoto mmoja mwenye umri wa miaka mitano anasadikiwa kubakwa katika eneo la Kabuholo kata ya Kirumba wilayani Ilemela ijini Mwanza na kijana mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa kisha kutokomea kusikojulikana.

Wakizungumzia tukio hilo baadhi ya wananchi katika eneo la tukio wamesikitishwa na kitendo hicho cha kikatili dhidi ya mtoto huyo.

“Kitendo cha kikatili jamani kwani sisi wakazi wa Mwanza tumekumbwa na nini hatuelewi kwani vitendo vya kinyama vimeshamiri tofuati na miaka ya zamani,” walisema Wananchi.Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi amesema kuwa kutokana na kijana huyo kufanya unyama huo kisha kutokomea kusikojulikana amesema jeshi la polisi linaendelea kumtafuta mtuhumiwa huyo na kwamba atakapokamatwa sheria itafuata mkondo wake.

Kamanda Msangi amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kuhakikisha mtuhumiwa huyo anatiwa nguvuni.

No comments :

Post a Comment